DAR ES SALAAM
Wamiliki wa Mitandao ya Kijamii ikiwemo Blogu Tanzania, leo wameadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani kwa kupinga kubaguliwa.
Hatua hiyo imekuja baada ya kutoshirikishwa walau mwanachama mmoja kutoka Chama Cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao hiyo, Tanzania Bloggers Network (TBN), katika Maadhimisho ya Siku hiyo yaliyofanyika Kitaifa leo jijini Mwanza.
IFUATAYO NI TAARIFA RASMI KAMA ILIVYOTOLEWA NA UONGOZI WA TBN
Chama cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Jamii nchini 'Tanzania Bloggers Network' – TBN inawaomba wanachama wake wote kutotumia taarifa ama habari au picha yoyote kutoka katika mkutano wa maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari (WPFD) unaofanyika kitaifa mkoani Mwanza.

Kamati Kuu ya Uongozi TBN imefikia hatua hiyo leo baada ya kujadiliana na kujiridhisha kuwa kumekuwepo na taasisi za tasnia ya habari ambazo zimekuwa zikiwatenga wanahabari wa mitandao ya kijamii (bloggers) na kutotambua umuhimu wao wakati sehemu kubwa ya taarifa mbalimbali nchini husambazwa na mitandao hiyo.
TBN iliyosajiliwa rasmi serikalini Aprili 2015 na kupewa namba ya usajili; S. A 20008 inawataka wanachama wake kutotoa ushirikiano wa aina yoyote kwa taasisi ambazo zinawatenga bloggers.
Tunasikitika kufikia hatua hii ila hamna jinsi. TBN itasikitika na kumshangaa mwanachama wake au blogger asiye mwanachama kutounga mkono agizo hili, na kwenda kinyume na agizo hili. Muda umefika ‘Bloggers’ kudai heshima, kutambulika na kuthaminika kama tasnia ya habari ingine yoyote.
Imetolewa na;-
Mwenyekiti wa Muda wa TBN
Joachim E. Mushi
03/05/2016
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269