Breaking News

Your Ad Spot

May 3, 2016

WANAJESHI WA UINGEREZA WATUA SOMALIA

Wanajeshi wa Uingereza wamewasili nchini Somalia kusaidia katika juhudi za kukabiliana na wapiganaji wa Kiislamu wa al-Shabaab.

Wanajeshi hao ni sehemu ya kikosi cha Umoja wa Mataifa.
Wanajeshi waliowasili Somalia ni 10 na watasaidia kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika (Amisom) kukabiliana na al-Shabaab.

Idadi ya wanajeshi wa Uingereza nchini Somalia inatarajiwa kupanda hadi 70 sana wakihusika na shughuli za matibabu, mipango na uhandisi.

Wapiganaji wa al-Shabaab wamekuwa wakikabiliana na serikali ya Somalia kudhibiti maeneo ya nchi hiyo.
Wamekuwa wakitekeleza msururu wa mashambulio ndani ya nchi na pia nje ya nchi, hasa katika nchi jirani ya Kenya.
Kundi hilo linakadiriwa kuwa na wapiganaji kati ya 7,000 na 9,000.

Kikosi cha Amisom kilizinduliwa mwaka 2007 na kina wanajeshi kutoka Uganda, Burundi, Djibouti, Kenya na Ethiopia. CHANZO NA BBC

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages