Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Meja Jenerali Projest Rwegasira (aliyevaa kiraia), akifafanua jambo kwa viongozi wa Idara ya
Uhamiaji Wilayani Nkinga, mara baada ya
kutembelea jiwe linaloonyesha mpaka kati ya Tanzania na Kenya katika kijiji cha
Jasini kilichopo Kaunti ya Kwale. Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya
kikazi ikiwa na lengo la kukagua na
kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.
.
(PICHA NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA
NCHI)
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja
Jenerali Projest Rwegasira(kushoto), akionyeshwa namba za jiwe la mpaka unaotenganisha
nchi za Kenya na Tanzania
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto), akisalimiana na maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama, mara baada ya
kuwasili katika kituo cha Uhamiaji Horohoro, wilayani Mkinga mpakani mwa Kenya
na Tanzania, barabara kuu ya Mombasa-Tanga. Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa
ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na
wahamiaji haramu kuingia nchini
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja
Jenerali Projest Rwegasira, akiweka saini katika kitabu cha wageni, mara baada
ya kuwasili katika kituo cha Uhamiaji Horohoro, wilayani Mkinga mpakani mwa
Kenya na Tanzania, barabara kuu ya Mombasa-Tanga. Katibu Mkuu yuko jijini Tanga
kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia
nchini
Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji Horohoro, DCI Deogratius
Magoma, akimuelekeza jambo Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja
Jenerali Projest Rwegasira mara baada ya ukaguzi wa ofisi za jengo la kituo
hicho zinazotumika katika utoaji huduma za uingiaji na utokaji wa raia wa
kigeni na raia wa Tanzania wanaopitia mpaka wa horohoro , wilayani Mkinga,
jijini Tanga. Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga, DCI Andrew
Kalengo, akimuelekeza jambo Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, mara baada
ya kutembelea daraja la Mwakijembe, linalotumiwa na wakazi wa nchi za Tanzania
na Kenya. Katibu Mkuu yuko jijini
Tanga kwa ziara ya kikazi
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269