Breaking News

Your Ad Spot

Jun 20, 2016

WAPINZANI WAMBADILISHIA STAILI NAIBU SPIKA ACKSON, LEO WAJIZIBA MIDOMO KWA VITAMBAA

Wabuge wa upinzani Leo Juni 20, 2016, wameongeza shinikizo la kumpinga naibu spika wa bunge Dkt.Tulia Jackson, kwa kujiziba midomo na vitambaa. Wabunge hao kama kawaida yao walisimama na kutoka bungeni pale naibu spika alipoketi kwenye kiti chake ili kuongoza Bunge hilo leo. Baadaye Mbuge wa jimbo la Vunjo, James Mbatia, aliwaambia waandishi wa Habari kuwa Kambi yaupinzani itaendelea na msimamo wake wa kupinga Uhuru wa kutoa mawazo na wataendelea kutoka bungeni endapo atakayekuwa akiongoza Bunge ni naibu spika Dkt.Jackson. Pichani mbunge wa Vunjo, James Mbatia akiongea na waandishi wa Habari huku akiwa amezungukwa na wabunge wa upinzani waliojiziba midomo kwenye lango la kuingilia bungeni Mjini  Dodoma Leo Juni 20, 2016.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages