Mhubiri na
Mwimbaji wa Muziki wa Injili nchini Tanzania, Masanja Mkandamizaji,
akihudumu katika Mkutano Mkubwa wa Injili wa Open Your Eyes and See OYES
2016 wenye lengo la kuwafungua watu wote kiroho na hivyo kuondokana na
vifungo mbalimbali vinavyowakabiri, uliofanyika katika Kanisa la EAGT
Lumala Mpya lililopo Sabasaba Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza.
Mkutano huo
ulianza June 12, 2016 na kufikia tamati jana June 19,2016 katika viwanja
vya Kanisa hilo. Wahubiri na waimbaji mbalimbali walihudumu katika
mkutano huo akiwemo Mchungaji wa Kimataifa kutoka nchini Canada Mama
Domitila Nabibone ambae amewahi kufariki na kufufuka siku ya nne,
Mwimbaji na Mhubiri Joseph Rwiza pamoja na Mwimbaji Chamwenyewe Jembe
ambapo watu wengi walifunguliwa kiroho na kuokoka katika mkutano huo.
Na George Binagi-GB Pazzo
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269