Zaidi ya akaunti 3,000 za benki za watu
wanaoaminika kuwa na mafungamano na harakati ya Hizbullah ya Lebanon
zinatazamiwa kufungwa karibuni hivi, kufuatia mashinikizo ya Marekani.
Gazeti la Asharq Al-Awsat linalochapishwa kila siku nchini
Saudia limeripoti kuwa, watakaoathirika na kufungwa akaunti zao za benki
ni pamoja na wafanyakazi, washirika na wateja wanaohusishwa na
Hizbullah.
Kufuatia mashinikizo ya Marekani, Riadh Salameh, Gavana wa Benki Kuu
ya Lebanon tayari ameagiza kufungwa akaunti 100 za watu wanaodaiwa kuwa
na uhusiano na Hizbullah. Hii ni katika hali ambayo, Mkuu wa harakati ya
al-Marada ya Lebanon amesema kuwa, vikwazo vya kifedha vilivyowekwa na
Marekani dhidi ya Hizbullah haviwezi kuidhoofisha harakati hiyo ya
muqawama wa Kiislamu. Amesisitiza kuwa, njama za Washington
kuzishinikiza benki na serikali ya Lebanon ili zikubali kushirinikiana
nayo katika vikwazo hivyo hazitosaidia kitu. Ameashiria kuwa, uzoefu
unaonesha kwamba vikwazo huwa na matokeo tofauti na yanayotarajiwa na
maadui na kwamba vikwazo vya hivi sasa vya Marekani dhidi ya Hizbullah
vitazidisha tu ushawishi na nguvu za harakati hiyo na kuifanya kuwa na
misimamo imara zaidi. Baada ya kupasisha vikwazo vya kifedha dhidi ya
Hizbullah kwa ajili ya kudhamini manufaa ya utawala wa Kizayuni wa
Israel na Saudia, serikali ya Marekani ilimtuma Waziri wake wa Hazina
mjini Beirut ili kuishinikiza serikali ya Lebanon ikubali kushirikiana
nayo katika vikwazo dhidi ya Hizbullah.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269