Katika kuelekea kilele cha Maonyesho ya
40 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Paul Makonda ametembelea banda la Umoja wa Mataifa (UN) lililopo katika
ukumbi wa Karume kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa
jijini Dar.
Makonda alifika katika banda hilo na
kupata nafasi ya kupata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa UN kuhusu kazi
ambazo zinafanywa na shirika hilo hapa nchini.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa
Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu (kulia) akitoa maelezo ya shughuli
mbalimbali zinazofanywa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini kwa Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati) alipotembea banda la
shirika hilo lililopo katika ukumbi wa Karume kwenye Maonyesho ya 40 ya
Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere
barabara ya Kilwa jijini Dar.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa
Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu kuhusu Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu
(SDGs) ambayo yanatakiwa kumfikia kila mwananchi alipotembelea banda la
Umoja wa Mataifa lillilopo katika ukumbi wa Karume kwenye Maonyesho ya
40 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu
Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa
Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu akimwonyesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDG's)
yaliyobandikwa katika banda la UN na jinsi walivyojipanga katika
kuelimisha wananchi kuhusiana na malengo hayo kwenye Maonyesho ya 40 ya
Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere
barabara ya Kilwa jijini Dar.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda akisaini kitabu cha wageni katika banda la Shirika la Umoja wa
Mataifa lililopo katika ukumbi wa Karume kwenye Maonyesho ya 40 ya
Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere
barabara ya Kilwa jijini Dar. Kulia ni Maafisa Habari wa Umoja wa
Mataifa, Hoyce Temu na Usia Nkhoma Ledama. RC Makonda amekuwa mgeni
kwanza mashuhuri kutembelea banda hilo na kutoa baraka zake kwenye
maonyesho hayo.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa
Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu katika picha ya pamoja huku wakiwa na
bango maalum linalowakilisha rangi za malengo 17 ya SDGs na mmoja wa
vijana aliyetembelea banda la Umoja wa Mataifa lililopo kwenye ukumbi wa
Karume kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea
katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar.
Afisa Habari wa kituo cha Habari cha
Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akizungumza na waandishi wa
habari kwa lengo la kuhamasisha wananchi kutembelea banda hilo na
kujifunza Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu SDGs na kujua shughuli
mbalimbali zinazofanywa na Shirika hilo hapa nchini.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269