Breaking News

Your Ad Spot

Jun 9, 2016

MKUU WA WILAYA YA KINONDNI AMTEMBELEA MZEE MWINYI LEO



Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi leo mchana ametembelea Rais mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es salaam.
Akiwa nyumbani kwa Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais mstaafu na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni walizungumzia mambo mbalimbali yahusuyo maendeleo ya Kinondoni na historia ya nchi kwa ujumla. Rais mstaafu alimshukuru Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni  kwa uamuzi wake wa kumtembelea na kumtakia kheri katika majukumu yake.
Aidha mh. Mkuu wa Wilaya alimshukuru Rais mstaafu Mh. Ali Hassan Mwinyi na kumtakia afya njema na maisha marefu.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages