Breaking News

Your Ad Spot

Jun 22, 2016

MUHIMBILI WATOA UFAFANUZI KUHUSU WAGOJWA WA SELI MUNDU

MSERU1Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Profesa. Lawrence Mseru akitoa ufafanuzi kuhusu habari iliyoandikwa na Gazeti la Mwananchi kuhusu huduma hospitalini hapo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Uuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Bibi. Agness Mtawa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Hospitalini hapo Aminiel Aligaesha.
Picha na: Frank Shija, MAELEZO.
………………………………………………………………………………………………………………
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru ametoa ufafanuzi kuhusu habari iliyoandikwa katika gazeti la Mwanchi la tarehe 21 Juni 2016 zilizo kuwa zinasema kuwa wagonjwa wa Seli Mundu wanalipishwa ili kupata huduma ya matibabu yao tofauti ilivyokuwa awali.
Akitoa ufafanuzi huo Profesa Mseru amesema kuwa kwa habari hizo siyo za kweli kwani wagonjwa wa Seli Mundu wanatumia utaratibu wa kawaida ambapo mgonjwa utibiwa katika maeneo wanayotoka na anapaswa kuchangia gharama za matibabu isipokuwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
Aliongeza kuwa hapo awali kulikuwa na mradi wa utafiti wa Seli Mundu ulioenda sambamba na utoaji wa matibabu kwa wagonjwa waliojumuishwa katika mradi huo uliodumu kwa muda wa miaka 10 hadi ulipofikia ukomo machi 30 mwaka huu.
Baada ya mradi huo kumalizika wagonjwa wote walirejea katika maeneo yao ambapo huko wanaendelea na matibabu kupitia utaratibu wa kawaida huduma za matibabu.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages