Benki ya kwanza ya Kiislam
nchini Tanzania Amana benki leo imezindua kituo chake cha huduma kwa wateja
ambacho kitakuwa kikiwasaidia wateja wake kuweza kupata taarifa mbalimbali
kuhusu huduma zao kama maulizo kuhusu bidhaa za amana, Atms,huduma za mitandao (simu
banking) na amana banki mtaani n.k.
Kituo hicho kitakuwa
kikifanya kazi kuanzia saa 2 asubuhi
mpaka saa 4 na watakuwa wanapatikana kwa nambari 0657980000 ambapo amana Bank
ni miongoni mwa benki zinazofanya vizuri kwa sasa wana matawi saba matano
yakiwa Dar es salaam,Arusha,Mwanza na wanatarajia kufungua matawi mengine mikoa
mingi zaidi ila waliyoipa kipaumbele zaidi ni Zanzibar na Tanga
Akizungumza na waadishi
wa habari meneja mfawidhi na huduma kwa wateja Juma Msabaha Amesema kuwa utaratibu
wanaotumia kuweza kuwapata mawakala ni
kwamba wakala lazima awe na leseni ya biashara pia awe na tin namba ya biashara
kuonyesha kuwa ni mlipa kodi pia awe amefanya
kazi zaidi ya miaka miwili na pia anaweza kuomba uwakala kwa namba zao ambazo
ni 0657980000 au info@ amanabank.co.tz na maombi yake yatapelekwa BOT kuweza
kujadiliwa na kama amekidhi vigezo atapewa uwakala ambapo amesema kuwa kwa sasa
wana mawakala kwa mikoa kama tabora ,bukoba,na mtwara na bado wanaendelea
kupokea maombi kutoka kwa watu mbalimbali.
Munir Rajab – mkuu wa
idarara ya biashara amana benki amisema kuanzishwa kituo hicho kuna lengo la
kuhitaji kuwa karibu na na wateja wao huku akitanabaisha kuwa huduma za kibenki huwa zinafanana lakini
kinachoweza kuwatofautisha ni ubora wa huduma kwa wateja na kwamba wao
wamejipanga vizuri kuingia kwenye ushindani huo ambapo wameamua kuwa mwaka huu
ni mwaka wa mawakala kwa sababu wanahitaji kuweza kuwafikia wateja wao mpaka
mahali ambapo hakuna matawi na wataweza kutumia huduma za kibenki kupitia
mawakala wao .
Mkuu wa biashara wa Bank ya AMANA nchini Tanzania Munir rajab akieleza mambo mbalimbali kwa wanahabari kuhusu huduma hiyo mpya kutoka kwao |
Bw. Juma Msabaha
akijibu swali wa muandishi wa habari Alisema kuwa utaratibu wanaotumia kuweza kuwapata mawakala ni kwamba wakala
lazima awe na leseni ya biashara pia awena tin namba ya biashara kuonyesha kuwa
ni mlipa kodi pia aweamefanya kazi zaidi
ya miaka miwili na pia anaweza kuomba uwakala kwa namba zao ambazo ni
0657980000 au info@ amanabank.co.tz na maombi yake yatapelekwa BOT kuweza
kujadiliwa na kana amekidhi vigezo atapewa uwakala . na kwa sasa wana mawakala
kwa mikoa kama Tabora ,Bukoba,na Mtwara na bado wanaendelea kupokea maombi
kutoka kwa watu mbalimbali.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269