NA K-VIS MEDIA NA VYOMBO VYA HABARI
HALI bado si shwari kwenye mataifa ya Ulaya baada ya watu wanane kuawa katika shambulio la risasi kwenye duka kubwa (Shooping Mall), Olympia, mjini Munich nchini Ujerumani leo Julai 22, 2016.
Polisi imethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kusema limeacha watu wengine kadhaa wamejeruhiwa vibaya.
Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari, msako wa kuwatafuta washambuliaji unaendelea ambapo mmoja kati ya watu hao wenye silaha ambao tayari polisi wameita shambulio hilo kuwa na “harufu” ya kigaidi alijipiga risasi kichwani na kufariki dunia baada ya kuzidiwa na polisi kwenye mapambano ya kurushiana risasi.
Mashuhuda wamesema, watu hao wameonekana wakiwa na bunduki tatu na tayari polisi imewataka wakazi wa mji huo kujiepusha na mikusanyiko na kubakia majumbani.
Wafanyakazi wa duko hilo bado wamo ndani ya jingo kaskazini magharibi wilaya ya Moosach na usafiri wa umma umesitishwa.
Kwa mujibu wa polisi, washambuliaji wanasakwa angani na ardhini, ambapo wadunguaji (Snipers), wanatumia helicopter kuwasaka washambuliaji hao
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269