Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban-Ki-moon akisalimiana na raisi Salva Kiir mjini Juba 25 februari 2016
Mapigano
mapya ya hivi karibuni nchini Sudani Kusini yaliyogharimu maisha ya
takribani watu laki tatu yanatarajiwa kutawala majadiliano ya mkutano
mkuu wa Umoja wa Afrika unaoanza jumapili katika jiji kuu la Kigali
nchini Rwanda.
Usitishwaji
wa mapigano umefanyika kuanzia jumatatu iliyopita baada ya kushuhudia
mapigano ya takribani siku nne mfululizo katika jiji kuu la Sudani
kusini Juba,ambapo mamia wamepoteza maisha na wengine arobaini elfu
kukimbia makazi yao.
Ghasia zilizoibuka zimeamsha shaka juu ya makubaliano ya amani yaliyokwama August 2015 kati ya pande hizo mbili.
Akizungumza
na wakuu wa Jumuia ya Maendeleo ya nchi za Mashariki na pembe ya Afrika
IGAD jumamosi mjini Kigali,katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon
alisema Sudani Kusini imefikia kiwango kibaya cha mzozo.
Akizungumza
kwa mara ya kwanza, rais Kiir amesema hataki tena kushuhudia umwagaji
damu nchini humo na kumtaka Machar kuwa karibu naye ili kwa pamoja
wakubaliane namna ya kuzuia mapigano kama haya katika siku zijazo.
Rais Kiir
ametoa kauli hiyo baada ya kukutana na kiongozi wa waangalizi wa
utekelezwaji wa mkataba wa amani rais wa zamani wa Bostwana Festus Mogae
na Mjumbe maalum wa Umoja wa Afrika nchini humo Alpha Oumar Konare,
katika Ikulu ya Juba.RFI
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269