Breaking News

Your Ad Spot

Aug 14, 2016

RAIS MSTAAFU DK KIKWETE ATOA TATHMINI YA JUMUIA YA MADOLA UCHAGUZI MKUU ZAMBIA

Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete akiwasilisha
 taarifa ya Timu ya Waangalizi wa
 Jumuiya ya Madola ya
 Uchaguzi Mkuu wa Zambia
Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete ametoa tamko la Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Madola  la Uchaguzi Mkuu wa Zambia uliofanyika tarehe 11 Agosti, 2016 kuchagua Rais, Wabunge, Mameya, Madiwani na Kura ya Maoni ya Katiba. Rais Mstaafu Kikwete yuko nchini Zambia kufuatia Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola kumteua kuwa Mwenyekiti wa Timu hiyo yenye waangalizi wa kimataifa 17 kutoka nchi za Jumuiya ya Madola.

Kwa mujibu wa tamko hilo, Jumuiya ya Madola imejiridhisha kuwa zoezi la upigaji kura, usimamizi wa kura na uhesabuji kura vituoni kwa ajili ya umeendeshwa kwa uwazi na kwa kuzingatia kanuni bora za uendeshaji wa chaguzi. Tamko linasema, dosari na hitilafu zilizojitokeza hazikuwa kubwa kiasi cha kuathiri matokeo ya uchaguzi mkuu huo.

Amewapongeza wananchi wa Zambia kwa kufanikisha zoezi la uchaguzi kwa amani na kutumia haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi wanaowataka. Amewasihi viongozi wa kisiasa wa Zambia, wagombea na vyama vya siasa kuheshimu maamuzi wa wananchi na pale inapojitokeza upande wowote kutoridhika na matokeo, zitumike njia za amani na kisheria za kutafuta ufumbuzi.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages