Mshambuliaji
wa Timu ya Simba, Laubit Mavugo akishangilia mara baada ya kuipatia
timu yake bao la Nne dhindi ya Wageni wao, AFC Leopards ya Nchini Kenya,
wakati wa Mtanange wao wa kirafiki ulioambatana na sherehe za
kuadhimisha Miaka 80 ya tangu kuanzishwa wa timu ya Simba a.k.a Wekundu
wa Msimbazi, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar
es salaam. Hadi kipenda cha mwisho kilipolizwa na Mwamuzi, Heri Sasi,
Simba ilikuwa ishaichakaza AFC Leopards kwa Bao 4 - 0.
Nahodha
wa Timu ya Simba, Jonas Mkude akiangalia namna ya kumtoka Mchezaji wa
Timu ya AFC Leopards ya nchini Kenya, Bernard Ongoma, wakati wa Mtanange
wao wa kirafiki ulioambatana na sherehe za kuadhimisha Miaka 80 ya
tangu kuanzishwa wa timu ya Simba a.k.a Wekundu wa Msimbazi, uliopigwa
jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam.Simba
imeshinda 4-0. NA OTHMAN MICHUZI
Mgeni
Rasmi katika Sherehe za kuadhimisha Miaka 80 ya Simba, Mkuu wa Mkoa wa
Dar es salaam, Paul Makonda akiongozana na viongozi mbali mbali wa Timu
ya Simba kuingia uwanjani kuwasalimia Wachezaji pamoja na Washabiki
waliofurika kwa wingi uwanjani hapo.
Wanamuziki wa Bendi ya Twanga Pepeta wakitoa Burudani uwanjani hapo.
TIMU
ya Simba imeibuka na ushindi mnono wa magoli 4-0 dhidi ya AFC Leopards
kutoka nchini Kenya, mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar
es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya miaka 80 ya tangu kuanzishwa kwa timu
ya Simba.
Simba
iliweza kutawala mchezo kwa kiasi kikubwa ambapo dakika ya 38 Ibrahim
Ajib aliipatia Simba bao la kuongoza baada ya kupokea pasi safi toka kwa
Jonas Mkude na kuachia shuti la chini chini umbali wa kama mita 25.
Kipindi
cha pili Simba iliwaingiza Muzamir Yassin, Jamal Mnyate na Laudit
Mavugo ambao walibadilisha mchezo kwa kiasi kikubwa kwa kuongeza
mashambulizi na kuwafanya mabeki wa Leopards kuwa 'bize' muda wote
kupambana na washambuliaji wa simba jambao ambalo lilishindwa kufua dafu
mbele ya washambuliaji hao.
Dakika
ya 55 Ajib tena anaifungia Simba goli la pili baada ya Mavugo
kuichambua vyema safu ya ulinzi ya Leopards na kumrahisishia mfungaji.
Dakika kumi baadae Kichuya alifungia Simba goli la tatu baada ya kupokea mpira wa krosi uliopigwa kiufundi na Mavugo.
Ilichukua
kama dakika saba hivi baada ya goli la tatu, pale Mavugo alipoifungia
timu yake goli la nne baada ya kumalizia kazi kubwa iliyofanywa na
Kichuya ambaye aliwafanya mabeki wa Leopards kuwa nae macho muda wote.
Mashabiki
wa Simba waliohudhuria mchezo huo wameonesha imani kubwa kwa kikosi
chao hicho kilichosukwa chini ya Omog kwa ushirikiano na Jackson
Mayanja.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269