Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda, akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa Kataa Unene Family (KUF), wakati wa maadhimisho ya miaka mitatu ya KUF yaliyofanyika jijini Dar es Salaam |
Kiongozi wa Kataa Unene Family Bi Angela
Msangi (katikati) akiwakaribisha wanachama wenzake wa Kataa Unene
Family wakati wa maadhimisho ya miaka mitatu ya KUF yaliyofanyika
Jumapili Agosti 7, 2016 jijini Dar es Salaam. Pembeni kulia ni Mjumbe wa
Kamati ya Nidhani ya KUF, Bi. Etty Kusiluka na Bi. Mariam Sagini
(kushoto) Mshindi wa shindano la kupunguza kilo 10 kwa muda wa miezi
mitatu.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akizungumza na wanachama wa
Kataa Unene Family (KUF) jumapili Agosti 7, 2016 wakati wa maadhimisho
ya miaka 3 tokea umoja huo kuanzishwa. Pembeni kulia ni Kiongozi wa
Kataa Unene Family Bi. Angela Msangi na Bi. Mariam Sagini Bi. Mariam
Sagini (kushoto) Mshindi wa shindano la kupunguza kilo 10 kwa muda wa
miezi mitatu.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akimsikiliza kiongozi wa KUF.
---
Kundi
la Kataa unene (KUF) linalojihusisha na kupunguza unene kwa mazoezi na
kula vyakula bora limeadhimisha miaka 3 kwa na kuweka mikakati mipya ya
kuwasaidia wengine.
Akizungumza
katika sherehe hiyo iliyofanyika Epidor Masaki, jijini Dar es Salaam,
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda ambaye alipita
kuwasalimia alilipongeza kundi hilo huku akisema kuwa afya ni msingi wa
maendeleo yoyote duniani, hivyo hatua ya kutambua kujiweka imara mapema
ni njema.
"Nawapongeza
sana kwa moyo mlionao wa kufanya mazoezi si jambo dogo maana linahitaji
nidhamu ya hali ya juu ... kujisimamia mwenyewe bila kushinikizwa na
mtu,' alisema Mhe. Makonda.
Aidha,
alieleza kuwa viwanja vya michezo jijini Dar es Salaam vipo vingi,
maeneo ya wazi pia hivyo kuwasihi wananchi kujihusisha katika mazoezi,
huo wao kama viongozi wakiwaunganisha na makundi mengine ya michezo kwa
mashindano kama Toto cup, Ndondo cup na mengineyo, hasa wanafunzi wa
vyuoni na shule za msingi.
Kwa
upande wake, Kiongozi wa Kataa Unene Family Bi Angela Msangi alisema
katika miaka mitatu, tayari watu zaidi ya 40 wamepunguza kuanzia kilo 15
hadi 25, ambapo tayari watu 10 wamefikia malengo ya kilo zinazohitajika
kutokana na urefu wao na wanaendelea kujidhibiti.
Angela
alisisitiza kuwa, kupungua kwa kufanya mazoezi na kula vyakula
vinavyofaa na kushauriwa kunawezekana endapo tu mtu ataamua kujikana na
kudhamiria,akiwaondoa watu fikra potofu kuwa wanaopungua wanatumia dawa.
Shughuli
hiyo ya Kataa Unene ilienda sambamba na kutoa zawadi kwa waliofanya
vizuri katika shindano la kupungua la miezi mitatu iliyopita, lililopewa
jina la Sagini challange,ambapo aliyeibuka kinara wa shindano hilo ni
muasisi wa shindano Mariam Sagini, aliyepunguza kilo 10 tangu mwezi Mei
mwaka huu.
Wanachama wa KUF wakimpongeza Mjumbe wa Kamati ya Nidhani ya KUF, Bi. Etty Kusiluka wakati akiwapa ujumbe.
Bi. Mariam akiwaonyesha wenzake jinsi gauni lake lilivyomkaa vyema baada ya kupungua kilo 10 kwa muda wa miezi mitatu.
"Yani mwenzako nimejaribu mara tatu"
Wanachama wa KUF wakibadilisha mawazo.
Wanachama wa KUF wakipongezana.
Wajumbe wa Kamati ya Nidhamu ya KUF, Bi.
Etty Kusiluka (kushoto na Bi. Ester Ulaya Cathbert (kulia)
wakibadilishana mawazo wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka mitatu.
Kila mwanachama aliweza kupata nafasi ya kuelezea changamoto na mafanikio yake.
Mjumbe wa Kamati ya Nidhamu Bi. Eter Ulaya Cathbert akitoa machache.
Wanachama wa KUF wakipeana zawadi.
Kiongozi wa Kataa Unene Family Bi Angela Msangi akitoa shukrani kwa wanachama wote walioweza kufika katika maadhimisho hayo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269