Bomu lililotegwa ndani ya gari, limelipuka na kuwauwa watu kadhaa katika mji wa Benghazi, nchini Libya.
Waliouwawa
wanasemekana kuwa wanaharakati wa kisiasa wanaofahamika na
wanaohusishwa na Jemedari mmoja anayeongoza kampeini ya miaka miwili,
dhidi ya wanamgambo wa Islamic State.
Mohammed Bou-qa-i-qis ameuwawa kwa pamoja na watu wengine wawili, huku wengine zaidi ya kumi wakijeruhiwa vibaya.
Mlipuko ndani ya gari
Amekuwa
akiendesha kipindi cha kila siku cha Runinga huku akiahidi kuwaunga
mkono wanaharakati wanaopinga kampeini za I-S, inayoongozwa na Jenerali
Khalifa Hafter.
Usalama katikati mwa mji wa Benghazi umeimarika pakubwa, lakini mapigano viungani mwa mji huo, bado yanaendelea,
Maiti ya watu 10 ambao hawajulikani, ilipatikana siku ya Ijumaa, ikiwa inaonekana waliteswa hadi kufa.BBC
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269