Brigedia Jenerali Salam
Naibu Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa
Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) amesema kuwa, Iran imesimama
kidete na ndiyo nchi yenye amani na usalama zaidi ulimwenguni
inapolinganishwa na ukubwa na aina ya vitisho na vikwazo vinavyozikabili
nchi mbalimbali za dunia.
Brigedia Jenerali Hussein Salami
amebainisha kwamba, Iran hii leo ina nguvu za kukabiliana na vitisho
vyote na imesimama kidete katika hilo na kwamba imejiandaa kikamilifu
kukabiliana na adui katika kiwango chochote kile.
Naibu Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa
Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (SEPAH) amesema kuwa, hii leo anga kwa
ajili ya ukoloni katika ardhi za Kiislamu imebanwa zaidi na ardhi hizo
zimegeuka na kuwa medani za jihadi za Waislamu.
Brigedia Salami amebainisha pia kwamba,
katika ardhi za Kiislamu ikiwemo Yemen ambayo imesimama kupambana na
utawala wa Aal Saud mpaka nchini Bahrain ambako Waislamu wameamka,
tayari kumejitokeza mapinduzi na kwamba ardhi hizo hivi sasa si mahala
salama tena kwa uistikbari.
Naibu Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa
Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (SEPAH) amezungumzia pia matukio ya
Iraq na kusema kuwa, wananchi wa nchi hiyo wamefanikiwa kudhibiti hali
ya mambo katika medani ya vita na kupambana na magaidi huku Hizbullah ya
Lebanon ikiwa fakhari ya ulimwengu wa Kiislamu inaendelea kuutikisa na
kuuteteresha utawala haramu wa Israel.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269