.

WANAFUNZI WAKWAZWA NA UHAMAJI HOLELA WA WALIMU- KIGOMA

Oct 8, 2016

Na Magreth Magosso,Kigoma

IMEFAHAMIKA kuwa,ubadilishwaji wa walimu katika shule za watu binafsi inachangia kwa kushuka kwa kiwango cha elimu kwa wanafunzi husika kutokana na  tatizo la walimu wanaopata ajira za muda katika shule hizo  huondoka  kwa muda mfupi, hali inayowaathiri kimasomo.

Kwa nyakati tofauti baadhi ya wanafunzi  Peter Lyoba kutoka shule ya sekondari Kibogora iliyoko wilayani Kakonko, na Lidia Shija shule ya Sekondari Bishop Mpango ya wilayani Kibondo Mkoani Kigoma wamesema kuwa kila mwalimu ana namna ya ufundishaji , hivyo kitendo cha ubadirishwaji wa walimu kila wakati  uwapa  usumbufu wa kuelewa ufundishaji wake.

`` shule binafsi wanategemea sana walimu wa muda ambao wengi  ukaa muda mfupi na kuondoka kutafuta ajira sehemu nyingine na wengine hurudi masomoni na atakayekuja anakuja na mtazamo mpya kwa kweli inatuboa ila ndo hatuna la kubadilisha mfumo wa elimu hasa tunaokosa nafasi shule za serikali ”walisema wanafunzi hao.

Akijibia hilo katika mahafali ya 10 ya kuhitimu wanafunzi wa kidato cha Nne shule ya sekondari ya Kibogora Mkuu wa kituo cha Seminary ya Iterambogo, Patrick Mahinja alisema kuwepo kwa walimu wa kudumu au wa muda si tatizo cha msingi ni kuwapata walimu  bora wanaojua  kazi na kuzingatia madili na weledi wa kufundisha wanafunzi.

Alipohojiwa mmoja wa walimu juu ya hilo Melesiana Leonidasi alisema sababu inayopelekea wengi wao kuhama na kuacha kazi kwenye shule binafsi ni kutokana na kutokuthaminiwa na  waajiri hasa pale wanapopata matatizo ya kifamilia ,hali inayopelekea kutafuata ajira serikalini ambako kuna mafao mtambukwa , licha ya mishahara mikubwa wanayolipwa katika shule hizo.

Akitetea hilo Makamu Mwenyekiti wa Chama cha wamiliki wa shule  na vyuo binafisi (MOAF)  Jeremia Gwegenyeza alisema  serika itoe uhuru wa ajira kama inavyotoa uhuru wa maswala mengine juu ya elimu na kuongeza kuwa wengi licha ya kufundisha wanatafuta nafasi mbalimbali serikalini kama vile uafisa elimu uratibu nafasi ambazo hazipo katika sekta binafsi.

Alisema wanatumia gharama kubwa kupata walimu kutoka nchi jirani kama  Kenya na Uganda huku wakishawishi serikali iliangalie hilo kwa jicho la tatu maana mtu mmoja kuja kufanya kazi hapa nchini humgharamia kiasi cha  dola 5000 na kuwatoa hofu wanafunzi juu ya hilo.
Mwisho.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช