Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani
shambulio lililofanywa dhidi ya askari wa kulinda amani wa umoja huo
huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa jana
Jumapili alielezea kusikitishwa kwake na mripuko wa bomu uliotokea Goma,
katika mkoa wa Kivu Kaskazini huko kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo na kuwataka viongozi wa Kinshasa kuwadhaminia
ulinzi askari wa kimataifa wa kulinda amani na kuwatia mbaroni mara moja
wahusika wa shambulio hilo.
Msemaji huyo wa Umoja wa Mataifa
amesema, kuna wajibu wa kuitia nguvu mikakati ya jeshi la serikali ya
Kongo na askari wa kulinda amani wa kimataifa ili kumaliza uasi nchini
humo.
Kwa upande wake, Maman Sambo Sidikou,
mkuu wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa nchini Kongo DR
amesisitizia wajibu wa kushirikiana viongozi wa nchi hiyo na askari wa
kimataifa katika uchunguzi wa suala hilo ili wahalifu waweze kupatikana
na sheria kuchukua mkondo wake dhidi yao.
Umoja wa Mataifa umesema kuwa, msichana
mmoja ameuawa na askari wawili wa kofia buluu yaani wa Umoja wa Mataifa
na raia wawili wamejeruhiwa katika mripuko wa bomu uliotokea magharibi
mwa mji wa Goma huko Kivu Kaskazini. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa,
askari wa kulinda amani wa kimataifa ndio waliolengwa kwenye shambulio
hilo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269