.

DANGOTE AFUNGA KIWANDA CHA SARUJI MTWARA, MITAMBO YAPATA KWIKWI

Nov 30, 2016

Mtwara
UZALISHAJI katika kiwanda cha saruji cha Dangote kilichopo Mtwara umeathirika kwa kiasi kikubwa tokea wiki iliyopita. Tatizo hili la muda limetokana na hitilafu za kiufundi katika mitambo ya kiwanda. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dangote Tanzania, Bwana Harpreet Duggal amesema mafundi wa Dangote wapo kazini na shughuli za uzalishaji zitarejea katika siku chache zijazo. 

Alisema kiwanda kilianza uzalishaji wa kibiashara mapema mwaka huu na kama ilivyo kwa kiwanda kingine kama hicho jambo lolote linaweza kutarajiwa hasa katika miezi ya mwanzo. Hata hivyo alizitaja hitilafu hizo kuwa ni za kawaida na uzalishaji utarejea katika kipindi kifupi kijacho. 

Alipoulizwa kuhusu gharama kubwa za uzalishaji, Bwana Duggal alisema unapolinganisha na gharama nyingine za uzalishaji katika Dangote, gharama za uendeshaji Tanzania ni za juu mno. Moja ya sababu kuu ni matumizi ya jenereta za dizeli katika kuendesha kiwanda. Na pia kiwanda kuwepo mbali na soko kuu la saruji kumechangia ongezeko la gharama za usafirishaji. Akasema serikali inaangalia suala hili la gharama na jinsi ya kutafuta njia ya kutupunguzia mzigo huu.

Akaongeza, “Tuna matumani makubwa kuhusu uwekezaji wetu wa muda mrefu hapa Tanzania na tupo makini, kwa kushirikiana na Serikali tutaweza kuhimili gharama za uzalishaji ili tuweze kuendelea kufanya bidhaa ya  saruji kuwa na bei nafuu nchini.”
Tangu kuzinduliwa kwa kiwanda cha saruji cha Dangote, bei ya saruji nchini Tanzania imeshuka kwa zaidi ya asilimia 30.


Kiwanda cha Dangote kilichopo Mtwara chenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 600 kina uwekezaji mkubwa katika saruji kuliko vyote katika Afrika Mashariki. Kina uwezo wa kuzalisha tani milioni tatu kwa mwaka na kutoa ajira ya moja kwa moja kwa zaidi ya watu 1000 wa Mtwara. 

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช