.

KUNDI LA WATU WENYE SILAHA LATIWA MBARONI BUNIA KONGO

Nov 17, 2016

Inspekta wa Polisi katika mkoa wa Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ameripoti kutiwa mbaroni kundi moja la watu wenye silaha katika mji wa Bunia nchini humo.
Joseph Alimasi Inspekta wa Polisi katika mkoa wa Ituri ametangaza kuwa kundi hilo lililokamatwa la watu 20 limepelekea kuhitimishwa mauaji katika mji wa Bunia makao makuu ya mkoa wa Ituri. Alimasi ameongeza kuwa askari usalama juzi Jumanne waliwaarifisha watu hao kwa Jefferson Abdallah Penembaka Gavana wa mkoa wa Ituri. Inspekta wa polisi wa mkoa wa Ituri amepongeza hatua hiyo ya askari usalama wa huko Bunia na kuwatolea wito wakazi wa mji huo kuendeleza ushirikiano kati yao na polisi.
Mji wa Bunia makao makuu ya mkoa wa Ituri huko Kongo DR
Hii ni katika hali ambayo baadhi ya wakuu wa taasisi za kiraia huko Kongo wamesema wana wasiwasi na kuwepo makundi ya watu wenye silaha katika mji wa Bunia. Maeneo ya mashariki na kaskazini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yanakabiliwa na ukosefu wa amani kwa miaka 20 sasa.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช