.

RAIS ASSAD: SINA IMANI NA TRUMP LAKINI AKIWA NA NIA YA KWELI YA KUPAMBANA NA UGAIDI, SYRIA ITASHIRIKIANA NAYE

Nov 17, 2016

Rais Bashar al-Assad wa Syria amesema kuwa, ikiwa Donald Trump, rais mteule wa Marekani atapambana kwa dhati na magaidi, basi serikali yake itashirikiana naye.
Rais Assad amefafanua zaidi kuwa, ikiwa rais huyo mteule wa Marekani atapambana na magaidi, basi atapata uungaji mkono wa nchi kadhaa kama vile Russia na Iran na nchi nyingine ambazo zinataka kuhitimisha wimbi la magaidi.
Donald Trump, rais mteule wa Marekani
Akijibu swali kuhusu matumaini aliyonayo kutoka kwa Donald Trump, Rais Assad amesema kuwa, hana imani na rais huyo mteule wa Marekani lakini angependelea rais huyo asiegemee upande wowote, aheshimu sheria za kimataifa, aache kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine na akomeshe uungaji mkono wa nchi yake kwa makundi ya kigaidi unaofanywa na serikali inayomaliza muda wake ya Rais Barack Obama.
Magaidi wenye misimamo ya Kiwahabi yanayotekeleza jinai za kutisha
Hayo yanajiri katika hali ambayo Trump ametangaza kuwa, amefikia natija kwamba Rais Assad ni chaguo bora na njia nzuri kwa ajili ya kupambana na ugaidi ambao umekita mizizi nchini Syria. Ni vyema kuashiria kuwa, magenge mengi ya kigaidi na ukufurishaji yanayotekeleza jinai za kutisha nchini Iraq na Syria yanapata himaya ya moja kwa moja kutoka serikali ya Marekani, utawala haramu wa Kizayuni wa Israel na baadhi ya nchi za eneo, hususan Saudia, Qatar na Uturuki.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช