Breaking News

Your Ad Spot

Nov 25, 2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA ATEMBELEA KIWANDA CHA MT. MERU MILLERS MJINI ARUSHA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na uongozi wa kiwanda cha Mt. Meru Millers mara baada ya kufanya ziara kiwandani hapo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mt. Meru Bw. Atul Mittal akitoa taarifa kwa Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan juu ya maendeleo ya kiwanda pamoja na changamoto wanazokutananazo wafanyabiashara wazawa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia malighafi zinazotumika kuzalishia mafuta ya kupikia kutoka kiwanda cha Mt. Meru Miller kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mt. Meru Bw. Atul Mittal akitoa ufafanuzi juu ya malighafi hizo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia malighafi zinazotumika kuzalishia mafuta ya kupikia kutoka kiwanda cha Mt. Meru Miller mjini Arusha.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akingalia ndoo za plastiki zinazotengenezwa na kampuni ya Mt. Meru Millers kwa ajili ya kuhifadhia mafuta ya kula ,kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mt. Meru Bw. Atul Mittal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inajipanga kuondoa utitiri wa kodi mbalimbali zinatozwa kwenye viwanda kama hatua ya kuviwezesha viwanda vingi nchini  kuongeza uzalishaji na kutoa ajira nyingi kwa watanzania.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo leo Jijini Arusha baada ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Mount Meru Millers ili kujua changamoto zinazokikabili kiwanda hicho ili Serikali iweze kuzifanyia kazi katika kuleta unafuu kwenye uzalishaji wa mafuta ya kupikia nchini.
Makamu wa Rais amesema mlolongo wa kodi zinazotozwa kwa wamiliki wa viwanda hazina uratibu mzuri hivyo mkakati ya Serikali wa awamu ya Tano inataka kuweka utaratibu mzuri wa ulipaji wa kodi hizo ikiwemo kuondoa kodi ambazo ni kero kwenye viwanda.
Amesisitiza kuwa Serikali ya awamu ya Tano imedhamiria kuhakikisha viwanda vingi vinajengwa nchini ambavyo vitatumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini hali ambayo itasaidia uuzaji wa bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi kuuzwa kwenye masoko ya nje ya nchi na kuliingizia taifa mapato na kuongeza ajira kwa makundi mbalimbali ya wananchi.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema ziara ambazo anafanya kwenye viwanda mkoani Arusha ni kujionea jinsi viwanda hivyo vinavyofanya kazi za uzalishaji na pale kwenye changamoto zinazokwamisha viwanda hivyo kufanya kazi vizuri ziweze kufanyia kazi na Serikali.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mount Meru Millers Atul Mittal amesema kama Serikali itafuta au kuondoa utitiri wa kodi wanazotozwa kwenye Viwanda hivyo watakuwa na uwezo wa kuongeza maradufu uzalishaji na kutoa ajira nyingi kwa Watanzania.
Amesema kwa sasa Kampuni hiyo inafanya kazi kwenye nchi 10 barani Afrika na kwa Tanzania pekee imeajiri wafanyakazi zaidi ya 1000 ambao wanafanyakazi katika maeneo mbalimbali nchini.(P.T)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages