Breaking News

Your Ad Spot

Nov 25, 2016

MAKONDA MOTO ILALA, CHANIKA KWAWAKA, MWENYEKITI WA MTAA ASWEKWA KITUO CHA POLISI KWA TUHUMA ZA KUUZA VIWANJA

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Zavala, Buyuni wilayani Ilala, Chiku Mwalufamba, akiwa chini ya ulinzi wa Polisi wa kike wakati akimpeleka kwenye Kituo cha Polisi cha Chanika, baada ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutoa amri ya Mwenyekiti huyo wa mtaa kushindwa kutoa maelezo ya kuridhirisha dhidi ya thuhuma za kuuza viwanja vya umma kiyume cha sheria, zilizotolewa na baadhi ya wananchi katika mkutao wa hadhara alioanya Makonda kweye viwaja vya Kituo cha Polisi cha Chanika, akiwa katika ziara ya kusikiliza na kuzitafutia ufumbuzi kero za wananchi, wilayani ilala, leo.
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Zavala, Buyuni wilayani Ilala, Chiku Mwalufamba, akingizwa kweye gari la Polisi chini ya ulinzi,
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Zavala, Buyuni wilayani Ilala, Chiku Mwalufamba, akiwa katika gari la Polisi akati wakati akimpeleka kwenye Kituo cha Polisi cha Chanika.


ZIARA ILIANZIA HAPA
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alianzia ziara yake kwa kukagua uendeshaji wa Kiwanda wa cha tambi cha TanzaniaPasta, kilichopo eneo la Viwanda, Vingunguti wilayani Ilala. akizungungumza alipongeza hatua ya kuanzishwa kiwanda hicho akisema kinachangia lengo la Rais John Magufuli la kutaka Tanzania ijayo kuwa ya viwanda kwa lengo la kukuza nakuimarisha uchumi wa Taifa.
  Hata hivyo aliutaka uongozi wa Kiwanda hicho kuhakikisha kinatimiza masharti ya utunzaji mazingira ikiwa ni pamoja na kutotiririsha maji hovyo, na pia kuhakikisha wananchi waliokusudiwa kulipwa ili kuondoka karibu na kiwanda wanafanyiwa hivyo mapema. Pia aliwaasa wananchi kusisitiza watoto wao kusoma masomo ya sayansi kwa kuwa kazi nyingi za viwandani zinafanywa na masomi wa somo hilo, na kwamba vinginevyo atakaoajiriwa bila kuwa na elimu ya sayansi watabaki kuwa waokota maboksi.
 Uongozi wa Kiwanda ukimtembeza makonda katika maeneo mbalimbali ya kiwanda. Kushoto ni Katibu Tawala wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo.
 Uongozi wa Kiwanda ukimtembeza makonda katika maeneo mbalimbali ya kiwanda. Kushoto ni Katibu Tawala wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo.
 Meneja uzalishaji wa kiwanda cha Tanzania Pasta Industries Limited, Imran Ul Rashid akiyooshamkono kumumpa maelezo Makonda iyekuwa akikagua shughuli za kiwanda hicho
 Baadhi ya ujumbe wa Makonda katika ziara hiyo Kiwandani 
Meneja uzalishaji wa kiwanda cha Tanzania Pasta Industries Limited, Imran Ul Rashid akiyooshamkono kumumpa maelezo Makonda iyekuwa akikagua shughuli za kiwanda hicho
Makonda akitazama hatua za mwisho za utengeezaji tambi katika kiwanda hicho
Uongozi wa Kiwanda ukimtembeza makonda katika maeneo mbalimbali ya kiwanda. Kushoto ni Katibu Tawala wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo.
Uongozi wa Kiwanda ukimtembeza makonda katika maeneo mbalimbali ya kiwanda.
Makonda akitazama tambi zinavyohifadhiwa katika makasha
Uongozi wa Kiwanda ukimtembeza makonda katika maeneo mbalimbali ya kiwanda.
Makonda akipata maelezo ya kina kuhusu uzalishaji na ubora wa tambi
Makonda akionyeshwa maboksi ya tambi


UKAGUZI WA UJENZI WA BARABARA KIWANGO CHA LAMI
Baadhi ya ananchi wakiwa kwenye barabara ya Segerea Bonyokwa ambayo ipo katika kujengwa kwa kiwango cha lami
DARAJA LA LINALOUNGANISHA BONYOKWA NA KINYEREZI
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alikagua pia ujenzi wa daraja linalounganisha Bonyokwa na Kinyerezi wilayani Ilala, ambalo ujnezi wake umekuwa ukisua sua kukamilika. Makonda ameiagiza kampuni inayofanya ujenzi huo kuhakikisha unakamilika baadaya siku 25 kuanzia leo. Vinginevyo hatua zaidi zitachukuliwa dhidi ya kampuni hiyo ya Alex, ikiwemo kutopewa kazi yoyote mkoani Dar es Salaam.
Hali ya daraja hilo
Mbunge wa Segerea Bona Kalua akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa araja hilo
Mkandarasi wa Kampuni ya Alex akitoa maelezo
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza baada ya kukagua soko la Kelezange lililopo Kivule ambalo linakabiliwa na mgogoro wa kuuzwa baadhi ya maeneo yao
Makonda akikagua daraja la Kivule kwa kupita na gari lake.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wananchi katika eneo la Ukonga, akiwa katika ziara hiyo. Aliwataka wananchi kwenda katika masoko maalum yaliyopangwa na kuacha kufanya biashara barabarani.


SHULE YA MSINGI YA KISASA ILIYOJENGWA NA SERIKALI

 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza baada ya kuzindua nyumba vya madarasa katika shule ya Msingi Maghorofani, Ukonga
 Baadhi ya madarasa ya shule hiyo
 Makonda akiondoka baada ya kuzindua madarasa hayo
Baadhi ya waandishi mahiri wa habari waliopo kwenye ziara ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO-theNkoromo Blog

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages