Mama
Thulisile Madonsela kutoka Afrika ya Kusini hii leo anatunukiwa tuzo ya
Ujerumani kwa bara la Afrika ya mwaka 2016 katika halfa itakayofanyika
mjini Berlin hapa Ujerumani kutokana na kupambana na rushwa.
Mama huyo
amepata umaarufu kutokana na msimamo wake mkali dhidi ya rushwa
alipokuwa anahudumu kama mlinzi wa maslahi ya umma nchini humo. Kashfa
alizofichua Madonsela zimemhusisha hata Rais wa Afrika Kusini, Jacob
Zuma.Huku raia wengi wa Afrika kusini wakiendelea kuishi katika lindi la
umaskini, wanasiasa wanaochukuliwa kuwa wala rushwa wameendelea
kujijengea utajiri. Rais Jacob Zuma ni miongoni mwa waliohusishwa na
kashfa kadhaa ikiwemo ile ambapo fedha za walipa kodi zilitumika
kukarabati makaazi yake binafsi. Aliyefichua kashfa hiyo ni Thulisile
Madonsela wakati huo akiwa anahudumu kama mlinzi wa maslahi ya umma.
Katika
mahojiano ya kipekee na runinga ya DW mjini Berlin, Thuli kama
anavyofahamika na Waafrika kusini wengi alisema halikuwa jambo rahisi
hasa kufichua kashfa hiyo ya rais Zuma kwani alipokea vitisho vingi.
"Rais Zuma amekuwa akipokea vizuri matokeo mengi ya uchunguzi, lakini
bila shaka mara mbili matokeo yaliyomuhusu, hakuyashughulikia kama
nilivyotarajia. Nilipokea vitisho kutokana na hilo si moja kwa moja
kutoka kwa rais au serikali bali washirika wake ambao walinitaka
kuzifutilia mbali kesi kuhusu kashfa hizo au nifanye uchunguzi wa kina,
lakini hakukuwepo na msingi wa kufanyika uchunguzi wa kina kuliko
tulivyokuwa tumeagizwa kufanya."
Pamoja na
wafanyakazi wake 300 mlinzi huyo wa maslahi ya umma alipokea malalamiko
ya raia wa kawaida ambao hawakuwa na uwezo wa kuwa mawakili. Takriban
malalamiko 40,000 yameshugulikiwa na bi Madonsela alipokuwa ofisini kwa
miaka saba na kati ya malalamiko hayo elfu 30 yalifanikiwa. Rais Zuma
alipomchagua mwaka 2009 alimtaka ahakikishe kuwa ofisi yake inakuwa
wazi kwa raia wote na kwamba atafanya kazi zake bila upendeleo wala
woga. Na tangu kupewa wadhfa huo Madonsela alifanya kazi bila kuchoka na
alidai wakati wote haki kutoka pande zote za watu wenye uwezo na wasio
nao. Na anasema hakikuwa kibarua rahisi."Ilikuwa mara nyingi ni vigumu
kwa watu kuelewa kuwa tunaweza kumuagiza afisa yeyote mkuu wa serikali
kufanya kitu na bila shaka kwa heshima."
Tuzo hiyo
anayoipokea Thuli Mandonsela hutolewa kwa mtu aliyetimiza vigezo
vinavyohimiza uhuru, demokrasia na haki za binadamu. Waafrika Kusini
sasa wanamtaka kujitosa katika siasa ili kuwatetea wanyonge wito
aliokataa mama huyo aliyezaliwa na kulelewa mtaa wa mabanda wa Soweto.(P.T)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269