Breaking News

Your Ad Spot

Nov 12, 2016

UZINDUZI WA MAJENGO MAPYA YA WODI YA WATOTO NA KINAMAMA WAFANYIKA ZANZIBAR

uz7
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Afya Mhe,Mahmoud Thabit Kombo mara alipowasili katika uzinduzi wa majengo mapya ya Wodi ya  Kinamama na  Watoto katika Hospitali ya Mnazi Mmoja .
uz1
/Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizari ya Afya Nd, Halima Maulid mara alipowasili katika uzinduzi wa majengo mapya ya Wodi ya  Kinamama na  Watoto katika Hospitali ya Mnazi Mmoja .
uz2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akifuatana na  Waziri wa Afya Mhe, Mahmoud Thabit Kombo pamoja na Viongozi wengine mara alipowasili katika uzinduzi wa majengo mapya ya Wodi ya  Kinamama na  Watoto katika Hospitali ya Mnazi Mmoja
uz3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Chumba cha kulelea Watoto wachanga wakati alipotembelea  majengo mapya ya Wodi ya  Kinamama na  Watoto katika Hospitali ya Mnazi Mmoja baada ya uzinduzi rasmi,(wa pili kulia) mwakilishi wa Ubalozi wa Uholanzi Teresia  Mcha  .
uz4
Baadhi ya mashine za kulelea watoto wachanga zilizomo katika jengo la watoto na kinamama wajawazito yaliyozinduliwa na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein .
uz5
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Hauklend Bw.Eivend Hansen wakikata utepe kuzindua jengo la Wodi ya Watoto wakati wa uzinduzi wa majengo mapya ya Wodi ya  Kinamama na  Watoto uliofanyika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja. 
uz6
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mwakilishi wa Ubalozi wa Norwaya Bw. Victor Mlundo wakati wa kuzindua majengo mapya ya Wodi ya Watoto Kinamama katika Hospitali ya Mnazi mmjoja uliofanyika.  [Picha na Ikulu.]11/11/2016. (P.T)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages