.

MANCHESTER UNITED YAICHAPA TOTTENHAM HOTSPURS

Dec 12, 2016


Manchester United
BAO la kwanza kwa Mchezaji Bora wa Bundesliga ya huko Germany Msimu uliopita katika EPL, Ligi Kuu England, Henrikh Mkhitaryan, Leo limewapa Manchester United ushindi wa 1-0 dhidi ya Tottenham Hotspur Uwanjani Old Trafford.
Manchester UnitedBao hilo lilipatikana Dakika ya 29 kufuatia Pasi safi ya Ander Herrera kunaswa na Mkhitaryan na kuachia Shuti lililotinga Wavuni.
Manchester UnitedPaul Pogba angeweza kuipatia Man United Bao la Pili lakini Frikiki yake iligonga Posti lakini Bao hilo pekee la Mkhitaryan limetosha kuipa Man United ushindi wake wa kwanza katika Mechi 3 za EPL ambazo walitoka Sare 1-1 na Arsenal, West Ham na Everton, Mechi ambazo zote walitawala na kustahili ushindi.

Hata hivyo, Mechi hii iliisha vibaya kwa Man United na Mkhitaryan baada kuumizwa na Rose wa Spurs Rafu ambayo Man United walidai ni Penati.
Manchester UnitedMchezaji huyo wa Kimataifa wa Armenia alitolewa Uwanjani kwa Machela.

Ushindi huu wa Man United umeikita Nafasi ya 6 wakiwa Pointi 3 nyuma ya Timu ya 5 Spurs na 6 nyuma ya Timu ya 4 Man City.

VIKOSI: Manchester United (4-3-3): De Gea, Valencia, Jones, Rojo, Darmian, Ander Herrera (Fellaini 90+5), Carrick, Pogba, Mkhitaryan (Bailly 84), Ibrahimovic, Martial (Rashford 72,). 
Akiba: Mata, Rooney, Blind, Romero.
Kadi: Valencia, Pogba, Mkhitaryan
Goli: Mkhitaryan 29

Tottenham Hotspur (4-2-3-1): Lloris, Walker, Alderweireld, Vertonghen, Rose, Wanyama, Dembele (Winks 67), Eriksen (Nkoudou 82), Alli, Son (Sissoko 57,), Kane. 
Akiba: Vorm, Dier, Wimmer, Davies.
Kadi: Wanyama, Walker 

Refa: Robert Madley (West Yorkshire)

Matokeo: Jumapili Desemba 11
Chelsea 1 - 0 West Bromwich Albion
Manchester United 1 - 0 Tottenham Hotspur
Southampton 1 - 0 Middlesbrough
Liverpool 2 - 2 West Ham United

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª