Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu utekelezaji wa sheria ya
EPOCA kulingana na mabadiliko yaliyofanywa katika Sheria ya Fedha No. 2
ya mwaka 2016, jijni Dar es Salaam.
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisisitiza
jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu umuhimu wa
Kampuni za Mawasiliano kujisajili katika Soko la Hisa kama Sheria
inavyoelekeza, jijni Dar es Salaam.
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amezitaka
Kampuni za Mawasiliano kukamilisha taratibu za usajili katika Soko la
Hisa la Dar es Salaam kwa kuuza asilimia 25 ya hisa zote kadri ya Sheria
ya Masoko ya Mitaji na Dhamana inavyoelekeza mwishoni mwa mwaka huu.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam, Prof. Mbarawa ametaja kampuni hizo kuwa ni zile
zenye leseni za mawasiliano zilizotolewa kabla ya tarehe 1 Julai 2016
kwa ajili ya Miundombinu ya Mawasiliano, Huduma za Mawasiliano, na
Huduma za Matumizi.
“Watoa
huduma wote wa Mawasiliano wajisajili na kuuza hisa zao kwa wananchi
ndani ya mwezi wa Disemba”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Ameongeza
kuwa kwa Kampuni zilizopata leseni baada ya tarehe mosi Julai, 2016
watatakiwa kutimiza sharti hilo la kisheria kwa kipindi kisichozidi
miaka miwili tangu kusajiliwa.
Waziri
Prof. Mbarawa amesisitiza kuwa Kampuni zitakazokiuka Sheria hiyo
zitachukuliwa hatua za kisheria kupitia kifungu cha 21 (C) cha EPOCA,
2010.
Aidha,
amewataka wananchi kutumia fursa hiyo kununua hisa hizo na kuwa sehemu
ya wamiliki wa makampuni ya Mawasiliano ili kuongeza kipato na kushiriki
katika maamuzi ya kampuni hizo.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano(P.T)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269