Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa
Chakula Duniani (WFP) limeonya kuwa kama litaendelea kukabiliwa na
matatizo litalazimika kusimamisha upelekaji misaada kwa maelfu ya
wakimbizi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.
WFP limezitaka nchi na mashirika yanayotoa misaada kuongeza
misaada yao ya kibinadamu kwa shirika hilo ili ufikishaji misaada na
huduma muhimu za maisha kwa wakimbizi wanaokabiliwa na hali mbaya nchini
Jamhuri ya Afrika ya Kati iweze kuendelea.
Uhaba wa fedha katika mwaka huu unaomalizika wa 2016 umeathiri sana
shughuli za ufikishaji misaada na utoaji huduma za kibinadamu wa Shirika
la Mpango wa Chakula Duniani; na ndiyo maana ni watu wapatao laki nne
tu kati ya wakimbizi milioni moja wanaohitaji misaada ya kibinadamu
katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wameweza kupatiwa misaada na shirika
hilo.
Tangu mwaka 2013 kufuatia kupinduliwa utawala wa rais wa wakati huo
Francois Bozize na wanamgambo wa kundi la Seleka, Jamhuri ya Afrika ya
Kati imekuwa ikishuhudia machafuko, mapigano na vita vya ndani.
Mapigano na mashambulio dhidi ya raia yamekuwa sababu ya kuvurugika
amani, kuuawa, kujeruhiwa na kubaki bila ya makaazi zaidi ya robo moja
ya raia milioni nne na laki nane wa nchi hiyo.
Hata hivyo tangu Rais Faustin-Archange Touadéra aingie madarakani
mwezi Machi mwaka kufuatia uchaguzi wa kidemokrasia, kiongozi huyo
amekuwa akisisitizia udharura wa kurejeshwa amani na usalama nchini
humo.../
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269