Breaking News

Your Ad Spot

Jan 4, 2017

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFANYA ZIARA WILAYA YA KIGAMBONI

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe.  Kasim Majaliwa akizungumza na watumishi wa halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni wakati wa Ziara yake ya kikazi Wilayani humo,  Dar es Salaam katika Ukumbi wa Sunrise Beach Resort iliyopo katika Wilaya hiyo na kuzindua WD ya akinamama wajawazo ya Zahanati ya Kisarawe 2 na kutembelea viwanda vya Watercom na Milkcom vilivyoko eneo la Kisarawe 2 katika Wilaya hiyo ya Kigamboni.

 Ilikuwa ni sehemu ya Ziara yake ya kukagua Maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam ambayo ilimfikisha eneo hilo ambako kunaviwanda vya maziwavya Dar Fresh na maji Safi  ya afya, Viwanda hivyo ni  Watercom na Milkcom. Kiwanda cha Milkcom Dairies LTD  huzalisha maziwa  mabichi na mgando asili katika vifungashio vya 250  mls na 500mls ya aina ya Dar Fresh pamoja na bidhaa nyingine inayochanganywa na maziwa kama vile maembe, matunda mchanganyiko, ndizi, chokolet na mtindi wa vanilla.



Watercom huzalisha maji safi asili ya aina ya Afya ambayo yanajazwa kwenye chupa za ujazo wa 300ml, 350ml, 500ml, lita 1.5, lita 12 na 19 ambayo husambazwa kitaifa kupitia mtandao wa usambasaji wa  Watercom  na mawakala binafsi.



 Huu ni ushuhuda fika wa mchango mchango wa kampuni mama ya Oilcom Group katika utekelezaji wa kauli ya Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli  kuhusiana na Tanzania ya Vi
  Waziri Mkuu,  Kasim Majaliwa akisalimiana na Msimamizi wa kiwanda cha maziwa na mashamba, Ally Mohamed
Mbunge wa Jimbo la Kigambani, Dk. Faustine Ndugulile akizungumza jambo na Kaimu Mkuu wa Chuo Cha JKT Kimbiji Meja. Josephat John kabla ya kuwasili Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika hafla ya kuzungumza na watumishi wa halmashauri
 Mbunge wa Jimbo la Kigambani, Dk. Faustine Ndugulile akifafanua jambo na likiwemo la Daraja la Nyerere kuwa na tozo kubwa na kuwafanya wenye magari kukimbia ambapo daraja hilo nimkombozi kwao



 Muuguzi Mkuu wa Zahanati ya Kisarawe 2, Bonavita Mwankemwa akimuelekeza jambo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mara baada ya kuzindua WD ya akinamama wajawazito ya kujifungulia   

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza jambo wakati alipokuwa akiwasalimia wakazi wa Kisarawe 2  mara baada ya kuzindua WD ya akinamama wajawazito
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Meneja wa Oilcom, Abubakari Faraji wakati alipokuwa akimshukuru kwa kukamilisha kazi ya ujenzi wa WD ya akinamama wajawazito  ya Kasarawe 2 ambayo alifika na kuizindua, wakatikati ni  Msimamizi wa kiwanda cha maziwa na mashamba, Ally Mohamed
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpongeza Mkurugenzi wa Shirika mama la makampuni ya OilCom Group, Saidi Nahdi (aliye vaa kanzu) na kumuahidi kuwa Serikali itampa ushirikiano wa kutosha na ataongea na mamlaka husika ili apate Umeme wa kutosha



 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipokuwa akondoka baada ya kuzindua WD ya akinamama wajawazito. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
 
KHAMIS MUSSA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Majaliwa Kasimu Majaliwa ametoa siku Tatu  kwa watumishi 10 ambao wamepewa uhamisho wa kazi toka wilaya Temeke kuripoti katika eneo la kazi katika  manispaa ya Kigamboni haraka iwezekanavyo kabla hawaja chukuliwa hatua za kinidhamu.

Mhe. Majaliwa ametoa agizo hilo leo katika ziara yake alipo kuwa akizungumza na watumishi wa halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni , na kuwataka watumishi hao kufanya kazi kwa bidii na kutimiza majukumu yao ipasavyo kwa kutembelea katika maeneo ya wananchi ili kutatua changa moto za wananchi.

Aidha  Waziri Mkuu amefuta posho zote za chai (bites alowences) kwa halmashauri zote na ame elekeza fedha hizo kupelekwa katika shughuli za miradi ya  Maendeleo  , na ameongeza kuwa serikali imeuda tume kuchunguza  mishahara ya watumishi ili waweze kuongezewa maslahi yao.

Pamoja na hayo Mhe.  Majaliwa amesema serikali itaajiri walimu 400  wa Masomo ya sayansi na hisabati ili kukabiriana na tatizo la upungufu wa walimu wa masomo hayo, na utaratibu unaendelea kufanywa  baada ya kubaini watumishi hewa serikali iweze kuaza kutoa Ajira.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages