Afisa wazamani wa Polisi nchini Philipine hii leo amedai kuwa Rais
Rodrigo Durterte alimuamuru yeye pamoja na maafisa wengine wa kikosi cha
mauaji kuwaua wahalifu na wapinzani wake wakati Duterte alipokuwa meya
wa mji wa Davao kusini mwa nchi hiyo. Arthur Lascanas afisa wa zamani wa
polisi nchini humo ameeleza katika mkutano na waandishi wa habari kuwa
kikosi hicho cha mauaji kilipokea kati ya dola 400 na 100,000 kwa kila
mauaji ya mtu mmoja yaliyotekelezwa kwa amri ya Durtete. Afisa huyo
amesema aliongoza mauaji hayo dhidi ya watumiaji na wafanyabiashara wa
madawa ya kulevya pamoja na wahalifu wa makosa madogodogo katika mji wa
Davao wakati Duterte alipokuwa Meya wa mji huo kwa zaidi ya miongo
miwili. Amesema miongoni mwa waliouawa ni pamoja na mtangazaji
anayepinga ukomunisti Jun Pala pamoja na ndugu wawili wa kiume wa afisa
huyo na kuwa anakiri kufanya mauaji hayo na anaomba radhi kwa Mungu.
Maelezo ya Lascanas yanatofautiana na na ushahidi wake aliotoa awali
mbele ya tume ya uchunguzi ambapo alisema mauaji hayo hayakufanyika.
Your Ad Spot
Feb 20, 2017
Home
Unlabelled
AFISA WAZAMANI WA POLISI ADAI KUTEKELEZA MAUAJI KWA AMRI YA DURTERTE
AFISA WAZAMANI WA POLISI ADAI KUTEKELEZA MAUAJI KWA AMRI YA DURTERTE
Share This
About khamisimussa77@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269