Breaking News

Your Ad Spot

Feb 14, 2017

ORODHA YA MAHAKIMU NA MAJAJI WALIOVURUGA KESI ZA WAUZA UNGA KUTUA KWA JAJI MKUU

Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini Rogers Sianga 
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
JAJI Mkuu anatarajia kupokea orodha ya majina ya mahakimu na majaji ambao wamevuga kesi za watu wanaotuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya.
Hayo ameyasema jana Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini Rogers Sianga wakati wa mkuatano wa viongozi mbalimbali wa kitaifa na waandishi wa habari ulioandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa ajili kupambana na dawa za kulevya.
Sianga amesema kuwa kesi zimevurugwa na mahakimu na majaji. hivyo wale wote wanaohusika watashitakiwa na hata wawe na mali ambazo wamezipata kwa biashara hiyo zitataifishwa.
Amesema kuwa watazunguka katika maeneo mbalmbali ya jiji la Dar es Salaam ili kuhakikisha mtandao huo unapatikana na kwenda hata Zanzibar na mbinu zote wanazijua katika kufanya biashara hiyo.nae Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemkabidhi orodha ya majina 97 wanaojihusisha na dawa za kulevya na kuongeza kuwa moto umewashwa dhidi ya watu wanaojihusisha na dawa za kulevya.Amesema kuwa kuna nyumba 200 zinajihusisha na kufanya biashara ya madawa ya kulevya hapa jijini ambapo wote hao watafikiwa katika operesheni.
Nae Mohamed Khalid TID , amesema kuwa sasa ni mnyama ambae yuko tayari kupambana nawatu wanaouza pamoja na kutumia dawa za kulevya na amerudi kwa kufanya kazi na kuongeza kuwa kuimba hakuhitaji dawa za kulevya.
Katika mkutano huo watu wawili wametakiwa kufika katika Kituo cha Polisi kati ambao ni Chidi Mapenzi, Ayuob Mfaume Kiboko.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages