Breaking News

Your Ad Spot

May 11, 2017

RAIS WA AFRIKA KUSINI JACOB ZUMA AWASILI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MWENYEJI WAKE RAIS DKT. MAGUFIULI



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru mgeni wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma mara baada ya kuzungumza na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam Mei 11, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mgeni wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma wakati wa Nyimbo za Mataifa mawili (Tanzania & Afrika Kusini)  zikipigwa katika viwanja wa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mgeni wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma wakati wakielekea kwenye ukumbi wa mkutano kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya Kimaendeleo yahusuyo mataifa hayo mawili ya Tanzania na Afrika Kusini.

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akikagua Gwaride la Heshima aliloandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akikagua Gwaride la Heshima aliloandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akipunga mkono wakati akiwasili Ikulu akiwa pamoja na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na mgeni wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma kabla ya kuanza mazungumzo yao Rasmi Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akipiga ngoma wakati alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo na mgeni wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma kabla ya kuanza kuzungumza na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akisoma hotuba yake wakati akizungumza na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.



NA BEATRICE LYIMO NA IMMACULATE MAKILIKA- MAELEZO
SERIKALI za Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania na Afrika ya Kusini zasaini mikataba mitatu ya ushirikiano katika sekta mbalimbali zitakazosaidia kukuza uchumi wa nchi hizo mbili.
 
Hati za mikataba hiyo  zimesainiwa leo Ikulu Jijini  Dar es Salaam wakati wa mkutano wa Marais  wawili Dkt. John Magufuli  na  Jacob Zuma  na waandishi wa habari.
 
Mikataba iliyosainiwa baina ya nchi hizo mbili  ni hati ya muhtasari  wa makubaliano ya mkutano wa tume ya pamoja ya Marais kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Afrika Kusini uliolenga kuboresha makubaliano yaliyofikiwa wakati wa mkutano huo.
 
Hati ya makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya Bi Anuwai kati ya Serikali ya Tanzania na Afrika Kusini, inayolenga kuboresha ushirikiano katika sekta ya wanyamapori na uhifadhi.
 
Huku hati nyingine ikiwa ni makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya uchukuzi kati ya Serikali ya Tanzania na Afrika Kusini uliolenga kuboresha ushirikiano katika sekta ya uchukuzi.
 
Akizungumza wakati wa mkutano huo Rais Magufuli alisema ziara ya Rais Zuma imekwenda sambamba na mkutano wa kwanza wa tume ya Marais ambapo ulibainisha baadhi ya maeneo ya makubaliano.
 
Rais Magufuli alisema kuwa maeneo ya makubaliano hayo yalilenga kuimarisha na kukuza ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji baina ya nchi hizi mbili na njia za kundoa vikwazo vinavyokwamisha biashara baina yao.
 
“Hali ya biashara ya Afrika Kusini nchini kwa mwaka 2016 ni takribani Tsh Trilion 2.4  na uwekezaji wake ni Dola za Kimarekani 803.15 milioni iliyopelekea kupatikana kwa ajira kwa watanzania 20,916”alisema Rais Magufuli
 
Rais Magufuli alitaja maeneo mengine ya makubaliano kuwa ni kushirikiana katika  sekta ya viwanda  ambapo amewakaribisha wafanyabiashara kutoka nchini Afrika Kusini ili kuwekeza  katika kujenga viwanda vya kusindika mazao na hivyo  kukuza uchumi.
 
Kwa upande wa Sekta ya miundombinu na nishati wamelenga katika kuimarisha reli ya kati na upatikanaji wa umeme, ambapo
 Rais Dkt.Magufuli amemwomba Rais Zuma kutumia ushawishi wake katika Umoja wa nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi (BRICS) ili kuisaidia Tanzania kupata mkopo kwa gharama nafuu, kwa lengo la kuendeleza ujenzi wa miradi ya reli ya kati na umeme.
 
Vilevile, Marais hao wamekubaliana kubadilishana uzoefu na wataalamu kupitia sekta ya utalii ikiwemo kuwakiribisha wawekezaji kutoka nchi ya Afrika Kusini kuwekeza  kwa kujenga hoteli za kitalii pembezoni mwa fukwe za bahari ya Hindi.
 
Maeneo mengine ya makubaliano ni pamoja na  sekta za madini kwa kubadilishana uzoefu na utaalamu, afya kwa kuwakaribisha wawekezaji katika ujenzi wa viwanda vya kutengeneza dawa, elimu, sayansi na teknolojia ambapo Rais Zuma amekubali kupokea wataalamu wa lugha ya kiswahili watakaofundisha Afrika Kusini.
 
Rais Zuma alisema wataendelea kuimarisha uhusiano uliopo baina ya nchi hizo mbili, ikiwa ni pamoja na kukuza umoja wa Afrika ili kuondoa vikwazo mbalimbali vinavyokabili bara hilo.
 
“Tumefurahi kusaini mikataba hiyo leo, pamoja na kupata taarifa ya mawaziri iliyojitosheleza katika kuainisha maeneo ya ushirikiano na utekelezaji wake itakayosaidia kuleta maendeleo katika nchi hizi mbili” alisema Rais Zuma
 
Rais Jacob Zuma anakamilisha ziara yake ya siku mbili leo usiku iliyolenga  katika kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizi mbili, ikiwa ni pamoja na kuanisha maeneo mapya ya ushirikiano yatakayochochea maendeleo kwa manufaa ya wananchi.




Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akizungumza jambo na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Rais Dkt. John Pombe Magufuli


Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mama Sizakele Zuma Mke wa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma mara baada ya kufika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam.


Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akifurahia jambo pamoja na Mama Sizakele Zuma Mke wa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma aliyeambatana na msaidizi wake Ikulu jijini Dar es Salaam.



Vikundi vya Matarumbeta vikitoa burudani wakati Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma alipowasili Ikulu jijini Dar es salaam. (PICHA NA IKULU)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages