Breaking News

Your Ad Spot

Jul 10, 2017

AITEL NA GSMA WANDAA MASHINDANO YA SULUHU ZA MFUMO A MALIPO YA PESA KUPITIA SIMU ZA MKONONI

DAR ES SALAAM.
Kampuni ya simu za mkoni ya Airtel Tanzania kwa kushirikiana na GSMA wameandaa mashindano ya suluhu za mfumo wa malipo ya pesa kupitia simu za mkononi ambayo yanafanyika jijini Dar es Salaam kwa mwaka wa pili mfululizo.
Mashindano hayo ambayo yamedhaminiwa na Airtel money na Comviva wakishirikiana na muungano wa mashirika ya simu za mkononi ulimwenguni GSMA yanajumuisha washiriki kutoka Africa. Wajasiriamali wa TEKNOHAMA kutoka Ghana, Kenya, Uganda na Tanzania watachuana kutengeza suluhu kwenye maeneo makuu matatu, yaani malipo kwenye sekta ya usafirishaji, mfumo wa malipo ya jumla (bulk payment )na mfumo wa malipo ya pochi ya Comviva na Airtel yaani ( Airtel Comviva mobile wallet).  
Tanzania imepata fursa ya kuandaa mashindano hayo kwasababu inajulikana kama kiongozi katika sekta ya simu za mkononi inayoongoza katika kujenga mifumo ya malipo ya simu ( mobile money payment) Hivyo ni fursa ya kipekee kwa wajisiriamali wa kitanzania kuweza kutengeneza suluhu za mifumo ya malipo ya simu za mkononi zitakazotumika barani Africa.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo, Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchunda alisema ushirikiano huu ni muhimu kwa vile unawezesha wajasiriamali wa TEKNOHAMA kuja na suluhu ambayo itaweza kusaidia kufanya malipo kupitia simu za... INAENDELEA>BOFYA HAPA 

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages