Breaking News

Your Ad Spot

Nov 17, 2017

MAWAZIRI WA TANZANIA, BURUNDI WAFANYA ZIARA KAMBI YA WAKIMBIZI NYARUGUSU MKOANI KIGOMA


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza katika mkutano na wakimbizi wa Burundi wanaoishi kambi ya Nyarugusu, iliyoko wilayani Kasulu, mkoani Kigoma. Katika ziara hiyo iliyokuwa pia na ujumbe kutoka Serikali ya Burundi, ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani na Mafunzo ya Uzalendo, Pascal Barandagiye, lengo ikiwa kukagua zoezi la urejeshaji wakimbizi hao makwao linavyoendelea

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali Marco Gaguti, akizungumza katika mkutano na wakimbizi wa Burundi wanaoishi kambi ya Nyarugusu, iliyoko wilayani Kasulu, mkoani Kigoma. Katika ziara hiyo iliyokuwa pia na ujumbe kutoka Serikali ya Burundi, ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani na Mafunzo ya Uzalendo, Pascal Barandagiye, lengo ikiwa kukagua zoezi la urejeshaji wakimbizi hao makwao linavyoendelea.

Wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi ya Nyarugusu, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) katika mkutano na wakimbizi hao, Katika ziara hiyo iliyokuwa pia na ujumbe kutoka Serikali ya Burundi, ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani na Mafunzo ya Uzalendo, Pascal Barandagiye, lengo ikiwa kukagua zoezi la urejeshaji wakimbizi hao makwao linavyoendelea

Mkimbizi wa Burundi anayeishi kambi ya Nyarugusu, iliyoko wilayani Kasulu, mkoani Kigoma Paul Ndalaizye., akitoa maoni kwa niaba ya wakimbizi wanaoishi katika kambi hiyo wakati wa Mkutano uliohutubiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Waziri wa Mambo ya Ndani na Mafunzo ya Uzalendo, Pascal Barandagiye (hawapo pichani), lengo ikiwa kukagua zoezi la urejeshaji wakimbizi hao makwao linavyoendelea.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiongozana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali Marco Gaguti (kushoto), baada ya kuwasili Wilayani Kasulu,mkoani Kigoma  kwa ziara ya kikazi.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Waziri wa Mambo ya Ndani na Mafunzo ya Uzalendo nchini Burundi, Pascal Barandagiye (kulia), wakipiga ngoma baada ya kuwasili katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu, iliyoko Wilayani Kasulu,mkoani Kigoma.(PICHA NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages