Breaking News

Your Ad Spot

Jan 3, 2018

DIWANI MWINGINE WA CHADEMA IRINGA MJINI AJIUZULU



Aliyekuwa  diwani  wa  kata ya  Kwakilosa  kupitia  Chadema Joseph Lyata akionyesha  barua  ya  kujiuzulu nafasi ya  udiwani  leo mbele ya  wanahabari  mjini  Iringa
Lyata  akionyesha  barua  ya  kujiuzulu kwake  Udiwani
Aliyekuwa   diwani wa kata ya  Kwakilosa  mjini  Iringa Joseph Lyata  akieleza  sababu za  kujiuzulu  kwake udiwani  leo  kulia  ni aliyekuwa  diwani wa Kihesa  Edga  Mgimwa aliyejiuzulu mwaka jana na  kushoto kada wa Chadema  Bw  Kimata  ambae  pia  alijiuzulu
Na MatukiodaimaBlog

KASI  ya  madiwani  wa  chama  cha  Demokrasia na  maendeleo  (chadema)  jimbo la  Iringa  mjini  kujiuzulu  imezidi  kuongezeka   na  kufikia madiwani sita   sasa  baada ya  aliyekuwa  diwani wa Kwakilosa  Joseph Lyata  na  aliyekuwa  diwani wa kata ya  Ruaha Tandesy Sanga kutangaza  kujiuzulu  nafasi hiyo  leo .

Wakati  Lyata  akizungumza na  wanahabari  mkoa  wa Iringa  kujiuzulu kwake Tandesy Sanga  amezungumza  na  wanahabari  mkoani  Dar es Salaam  juu ya  kujiuzulu  kwake leo .

Akitangaza  azma  ya  kujiuzulu kwake  nafasi hiyo   mbele ya waandishi  wa  habari Lyata  amesema  kuwa  kujiuzulu  kwake  kumetokana na mahusiano mabaya  ya  kufifisha maendeleo kati  yake na  viongozi wa  juu wa Chadema  hicho akiwemo  mwenyekiti wa kanda ya  Nyasa Mchungaji  Peter  Msigwa  ambae  ni  mbunge wa   jimbo  la  Iringa mjini pamoja  na  uongozi wa juu wa Chadema  ukiongozwa na mwenyekiti  wake  Taifa Freeman  Mbowe.

Lyata  alisema  kuwa  mara kwa mara  amekuwa  akiandika  barua  kwa  uongozi wa  juu wa Chadema  Taifa   kuelezea  malalamiko yake ya  mahusiano mabaya kati yake na  mbunge wa  jimbo la  Iringa mjini Mchungaji Msigwa  ila wamekuwa  wakipuuza na  kuwa hajaona  sababu ya  kuendelea  kubaki ndani ya  chama  hicho  japo  safari yake ya  siasa  itaendelea  kupitia  chama  chochote ikiwezekana  hata  CCM .

"  Vyama  vya  siasa  vipo  vingi  kuna  CUF , ACT  Wazalendo  na  CCM  hivyo  nitachagua  ni  chama gani  kitanifaa  kufanya  siasa  zangu ila  hata  CCM nipo  tayari  hakuna  ubaya "

Alisema  kuwa figisu  figisu kati  yake  na  mbunge  Mchungaji Msigwa  zilianza toka  akiwa naibu meya  wa Manispaa ya  Iringa na  hofu ya mbunge  Msigwa  ni baada ya  kuhisi kuwa anautafuta  ubunge wa  jimbo  hilo mwaka  2020 .

"  Mbunge alikwenda katika  chombo kimoja wapo  cha  utangazaji mjini  Iringa (Radio jina limehifadhiwa ) na  kutangaza  kuwa Lyata  anautafuta  ubunge kwa  nguvu na hata  wezi  ila  niwa  wazi  sioni  kosa la  kuzuiwa  kugombea  ubunge  nikitaka na muda  ukifika  nitagombea   ila  namhakikishia  kuwa sijaondoka  katika  Chadema kutokana na kununuliwa nimeondoka  kutokana na mahusiano mabaya  kati yangu na mbunge Mchungaji Msigwa na  wapo  wengi  wanataraji  kuondoka na kujiuzulu nafasi zao  za  udiwani " alisema  Lyata

Kuwa  mchakato  wa  kumpata  naibu  meya  Manispaa ya  Iringa nafasi  ambayo  alikuwa  akiwania  mbunge aliweza  kuingilia mchakato   huo  na  kupanga  mtu  ambae  alimtaka  na  malalamiko  yake  alifikisha  ngazi  za  juu  ila  walikaa  kimya  huku  uongozi wa kanda  kuptia  katibu   wake ulimpuuza kabisa na  kuishia  kusema kuwa ni msaliti .

" Uchaguzi   mdogo wa udiwani Kimala Kilolo na  Kitwiru  mimi na Frank  Nyalusi  hatukupangwa  kushiriki kampeni Kitwiru  kwa  hofu ya  kutujenga  kisiasa  katika mbio za ubunge  tulipangwa Kilolo ila  kata  yangu  imepata maafa  ya nyumba  kuezuliwa  mbunge  hadi  sasa pamoja na kuwa na taarifa  hakuweza  kufika  aliyefika ni mkuu wa mkoa na mkuu wa  wilaya  ambao  waliweza  kunisaidia hadi  kuezeka nyumba   za  wananchi wangu ila mbunge badala ya  kushukuru  ameishia  kunilaumu  kuwa  kwanini nimeezeka nyumba na pesa nimepata wapi "

Hata   hivyo  Lyata  alisema  kwa  ajili ya kuonyesha ana  nguvu ya  kisiasa  kuliko  mbunge Mchungaji Msigwa ataendelea kufanya  siasa  na  kuwa suala la ubunge 2020 asubiri  muda  ufike  ila nyuma  yake  kuna  kundi  kubwa ya madiwani  na  viongozi wa chadema  watakaomfuata bila  kutaja majina  na  idadi yao  alisema  anaungwa mkono  na  madiwani  hao kwa uamuzi  wake .

Kuhusu  tuhuma  za  kununuliwa na  CCM kwa  zaidi ya  milioni 200 Lyata  alisema hajanunuliwa na kama amenunuliwa basi ni  mmoja  mwa  viongozi  wenye  sifa  kuzidi  ya  hao  wanaoeneza uvumi huu maana anayenunuliwa ni  yule anayekubalika na  aliyejiweka  jikoni kama  mmoja kati ya madiwani wa Chadema  ambae amekuwa  akieneza  uvumi ila huku  akitafuta  kununuliwa na  wana CCM

Kwa  upande  wake  Edga  Mgimwa  aliyekuwa  diwani wa  Kihesa  alisema  kuwa amevutiwa na kujiuzulu kwa Lyata  na  kuwa katika mkakati  wake  wa   kufanya kazi kama  kada wa CCM  jimbo la  Iringa ni madiwani  wengi  watajiuzulu .

Mbali ya Lyata na  Mgimwa  madiwani  wengine  waliojiuzulu kwa mwaka  jana na  sasa ni aliyekuwa diwani wa kata ya  Kitwiru  kupitia  Chadema  Baraka  Kimata  ambae  ni diwani  tena wa kata  hiyo  kupitia  CCM , pia  wapo madiwani  wa  viti maalum  wawili Husuna  Ngasi na Leah  Mleleu .

Mapema  mwaka jana akizungumza na  wanahabari mjini hapa  juu ya kujiuzulu kwa madiwani  wanne mwenyekiti wa kanda ya  Nyasa Mchungaji Msigwa  ambae ni  mbunge  wa  jimbo  hilo  alisema  kuwa kuna  mkakati wa CCM kuendelea  kununua madiwani na  kukanusha malalamiko ya madiwani hao  kuwa yeye  ni  chanzo cha  wao kujiuzulu kwao .

Huku naibu  meya  wa Manispaa ya  Iringa  Dady  Igogo  alisema  kuwa chama  kimewanunulia  vifaa maalum   kwa  ajili ya madiwani wa Chadema wanaonunuliwa  kurekodi mazungumzo  ya  kununuliwa  kwao .



No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages