.

SABABU TATU ZA CHINA KUDHIBITI MITANDAO YA KIJAMII, NA SOMO LA KUJIFUNZA TANZANIA

Mar 3, 2018

Na Daniel Sarungi-Information Security Expert (ISO)

Kabla hatujaanza, embu tuangazie tovuti zipi ambazo zimedhibitiwa vikali nchini China,

Google, Blogger, Flickr, MySpace, YouTube, Plurk, Wikipedia, HotMail, MSN, Live Search, Bing, Twitter, Facebook, Instagram, Snapchat n.k

Tuvoti tajwa hapo juu na zingine nyingi hazifanyi Kazi katika nchi ya China.

Napenda twende hatua kwa hatua ili tukimaliza uone ni kwa jinsi gani Tanzania tunaweza kufaidika na mfumo kama huo wa China.

Zifuatazo ni sababu Tatu zilizopelekea nchi ya China kudhibiti mitandao ya kijamii na tuvoti nyingi maarufu Duniani.

1. USHINDANI WA KIBIASHARA NA KODI

Makampuni makubwa yanayoendesha mitandao ya kijamii hawalipi kodi China kwasababu sio kampuni zinazoendeshwa ndani ya China.

Ni kama watanzania wengi wanavyotumia kampuni kama za Instagram, YouTube n.k huku Serikali ikiwa haipati kodi yoyote kutoka kwa kampuni hizo kwasababu ni kampuni zinazofanya shughuli zake nje ya Tanzania.

China ilitaka kutengeneza Pesa nyingi Zaidi hivyo waliamua kutengeneza mitandao yao ya kijamii ambayo itakuwa inalipa kodi.

*Badala ya Google, China ilitengeneza Baidu

*Badala ya Wikipedia, China ilitengeneza Hoodong

*Badala ya Blogger China ilitengeneza Blogcn

*Badala ya YouTube , China ilitengeneza Youku

*Badala ya Facebook, China ilitengeneza Renren

*Badala ya Gmail, China ilitengeneza QQmail na kadhalika

Kampuni zote hizo za China zinalipa kodi kwa serikali ya China, pia zinatoa ajira ikiwemo pamoja na kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja.

Ili kufanikisha kampuni za wazawa iliwalazimu Kufungia mitandao ya nje ya nchi maana haikuwa na faida kwa nchi ya China hasa katika kodi.

Kutokana na utamaduni na uzalendo wa nchi yao, wachina wamejikuta wakipenda vya kwao.

Mfano: Licha ya mtandao wa WhatsApp kuwepo China, wananchi wengi wamejikuta wakitumia weChat badala ya WhatsApp kwa sababu weChat imetengenezwa na wachina wenyewe

2. TAARIFA NYETI

Hii ni sababu ya msingi ya pili iliyofanya China kudhibiti tuvoti nyingi za nje. Tuvoti kama Blogger.com kwasababu zinakuwa hosted na kampuni za nje ya China, watu wanaweka taarifa mbaya kwa serikali ambayo inachangia kuharibu picha halisi ya China, hii inaweza kuleta athari kubwa kiuchumi ikiwemo kukosa watalii, wawekezaji n.k

Moja ya vitu ambavyo China inalinda kwa gharama zote ni heshima yao kama Taifa ndani ya mataifa mengine na haiwezi kuruhusu kuathiriwa kwa namna yoyote ile.

Tuvoti hizo pia ambazo ndizo zinazotumiwa kuangalia picha za ngono ambazo zinamomonyoa maadili na utamaduni wa Taifa.

3. USALAMA WA NCHI NA TAIFA
Serikali ya China haikutaka watu kuianika nchi yao kimataifa katika kujadili mambo mbali kuhusu siasa, viongozi wa kiserikali katika mitandao ya kimataifa kwasababu kwa kufanya hivyo Kunaweza kuleta athari na kuvuruga Amani katika nchi.

Mfano Mdogo kwa Tanzania ni hamasa inayoendelea kwenye mitandao ambapo watu wanaendesha kampeni za Maandamano ya tarehe 26/04 ambayo ni sikukuu ya Taifa ya Muungano, tunategemea kuwa na wageni mbali mbali kutoka mataifa mbali mbali, kwa Bahati mbaya Serikali yetu pendwa haiwezi kudhibiti mitandao hiyo kwasababu shughuli zake haziendeshewi hapa nchini badala yake Serikali inajipanga kushughulika na watakaoandamana kijeshi, jambo ambalo litaweza kuwa na athari kubwa sana kwa nchi yetu.

Maandamano hayo yanayofanywa Dunia nzima, tayari nchi za ughaibuni zimeshatoa kibali kwa watanzania watakaoandamana katika nchi hiz, huku Maandamano yakiendelea kusukwa kufanyika nchi nzima kila Mkoa na Wilaya.

Ndugu zangu napenda kuangazia na kushauri yafuatayo;

Vijana na wataalamu wetu waliosoma teknolojia wanaolalamika kwamba hakuna ajira, kweli wanashindwa kutengeneza mitandao mbadala ya kijamii ambayo itafanya kazi Duniani kote kutokea hapa Tanzania ili tuwe na mbadala? Sasa hivi tuna wabunge wameyakimbia majimbo yao, wametengeneza majimbo mtandaoni ili kuwafurahisha wafadhili Wao huko ughaibuni, ndugu zangu, Taifa linapoelekea tunahitaji maamuzi sasa, tuje na mbadala wa mambo ya mitandao.

Ni kweli hatukujiandaa kama Taifa kupokea teknolojia, lakini hatujachelewa. Tuchukue hatua sasa.

Taarifa nyingi za Serikali zinatumwa kupitia gmail account za watumishi wa serikali, mtandao wa mabepari ambao wanasoma kila kitu kinachotumwa kupitia mtandao Wao.

Wakati mwingine tunawasingizia watumishi kutuma data kwa Mange kumbe ni taarifa kupitia email tunazotumia.

Nashauri watumishi wote wa Umma watumie domain name/official email katika mawasiliano yote

Mfano:
Wizara ya Fedha:
daniel.sarungi@mof.go.tz badala ya @gmail.com au yahoo, iwe mandatory kwa kila mtumishi na ukiwa ofisini *FireWall* ikuzuie kufungua mtandao binafsi kama gmail n.k

Nashauri Serikali iangalie jinsi ya kudhibiti mitandao ambayo hailipi kodi kwa Taifa letu lakini pia zinatumika kama njia za kuvuruga amani

Naiomba serikali kuchukua hatua haraka kabla ili kuzuia Maandamano badala ya kusubiri kupambana na waandamanaji, wananchi wasio na hatia wanaweza kupoteza maisha kutokana na mvurugano huo.

Information is Power (rejea ujenzi wa mnara wa babeli, ulishindwa kuendelea baada ya kushindwa kuwasiliana)

When threat hits home, It's time to fight back

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช