.

MPINA AFUFUA KIWANDA CHA NYAMA SHINYANGA

Apr 10, 2018

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina  akiangalia moja ya sehemu ya jengo la Kiwanda cha nyama cha Shinyanga  iliyoharibiwa  na  kutolewa  mabomba  ambapo pia vitasa vya mlango vimetolewa alipofanya ziara ya kushitukiza katika kiwanda hicho leo.  (Picha na John Mapepele)
Na John Mapepele, Shinyanga 
Waziri  wa Mifugo na Uvuvi,  Luhaga Mpina  ametoa siku saba  kwa wawekezaji wa kiwanda cha nyama cha Kampuni ya Triple S Beef Limited na Agri Vision  kuwasilisha  hati zote  za umiliki  hati ya eneo la  kiwanda na eneo la kuhifadhia mifugo baadha  ya kushindwa kukiendeleza kwa miaka 11.

Akizungumza katika kiwanda hicho leo Mpina amuagiza Mkurugenzi wa Ubinafsishaji  na Ufuatiliaji Jones  Mwalemba kutoka Hazina kuhakikisha kwamba ifikapo Juni 30 mwaka huu kiwanda hicho kiwe kimempata mwekezaji  ambaye ataanza kazi mara moja ya uchinjaji  ili kutoa ajira na kuliingizia taifa mapato.

Aidha amemuagiza Msajili  wa Hazina  kuanza uhakiki wa mali zote za kiwanda hicho baada ya kubainika  wizi uliokithiri katika kiwanda hicho. 

Pia  Mpina ameamuru mmliki  wa Kampuni inayolinda kiwanda hicho kukamatwa mara moja na kufikishwa katika mikono ya sheria kwa ajili ya kujibu  mashitaka wa wizi  wa mali za kiwanda hicho ambapo  amemtaka Mkuu wa Mkoa  kuhakikisha kuanzia sasa kiwanda hicho kilindwe na  vyombo vya Serikali  badala ya makampuni binafsi.

Waziri Mpina alisema hatua ya Kampuni ya Triple S kuuza kiwanda  na kuingia mkataba mpya na  Kampuni  ya Agrovisioni ni kinyume  na mkataba wa awali ilioingia na Serikali.

“Huu ni ukiukwaji wa masharti ya Mkataba  kulingana na kifungo cha 16.1  ambapo sasa kinauondoa umiliki wake  katika kiwanda hiki” alisisitiza Mpina

Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Lovince Asimwe  kiwanda kilianza ujenzi wake mwaka 1975 na kwamba kimegharimu  dola za kimarekani milioni tatu na kilijengwa na Serikali kwa ufadhili wa Benki ya Dunia.

Alisema mwaka 2007 kiwanda hicho kilibinafsishwa kwa mwekezaji  Tripple S Beef Limited  lakini kutoka na na matatizo ya uendeshaji kiwanda hicho kilifungwa mwaka 2017 na kukabidhiwa kwa Serikali.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª