WATUHUMIWA wa kesi ya mauaji ya marehemu Swetu Fundikira, MTM 1900 Sajenti Roda Robert (42) wa kikosi cha JKT, Mbweni na MT 75854 Koplo Ally Ngumbe (37) wa JWTZ, Kunduchi wakiwa chini ya ulinzi wa polisi kwenda chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam mchana huu.
MTM 1900 Sajenti Roda Robert (42) JKT, Mbweni na MT 75854 Koplo Ally Ngumbe (37) wa JWTZ Kunduchi wakiwa wakisubiri kusomewa mashitaka katika mmahakama hiyo leo mchana.
STORY KWA UFUPI......
WATU wawili wanaosemekana kuwa ni mtu na mkewe ambao ni wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Weananchi wa Tanzania, mchana huu wametinga kizimbani katika mahakama ya Hakim Mkazi Kisutu dar es salaam, kwa tuhuma za kumua Swetu Fundikira kwa kipigo.
Washitakiwa hao MTM 1900 Sajenti Roda Robert (42) JKT, Mbweni na MT 75854 Koplo Ally Ngumbe (37) wa JWTZ Kunduchi, Dar es Salaam wamefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Geni Vitus Dudu na mashtaka yameendeshwa na wakili wa serikali Monica Mbogo aliyekuwa akisaidiwa na Beatrice Mpangala
Dudu aliwaeleza washitakiwa hao kwamba kwa mujibu wa kosa linalowakabili hawatakiwi kujibu chochote na kwamba kosa hilo halina dhamana kwa sababu hiyo mahakama haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo isipokuwa Mahakama Kuu. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februali 10 mwaka huu, itakapotajwa.na wsshitakiwa wamerejeshwa rumanade.
Kesi hiyo ilionekana kuwa na mvuto kutokana na wananchi wengi kuingia katika chumba cha mahakama kwa shauku ya kusikiliza kilichokuwa kikijiri kuhusu kesi hiyo.
Swetu alifariki dunia Jumapili asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alilazwa Ijumaa usiku baada ya kupigwa na watatu wanaodaiwa kuwa ni wanajeshi wa JWTZ, ambapo hadi sasas wamefikishwa mahakamani wawili na mmoja bado anasakwa na polisi. mwili wa marehemu Swetu ulizikwa jana kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar.
CIAO
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269