MKURUGENZI wa Sauti za Busara, Yusuf Mohammed akizungumza na mtangazaji wa TBC1 Evance Muhando katika hoteli ya Southern Sun, Dar es Salaam, leo katika mkutano wake na waandishi wa habari kutangaza tamasha hilo.
STORY
Ukiachana na hali mbaya ya kiuchumi ya Dunia iliyoathiri bodi ya Utalii, na ukosefu wa umeme wa muda mrefu, tangu kati kati ya Desemba mwaka jana, hatimaye kuna mtazamo chanya juu ya Tamasha la saba la muziki la Sauti za Busara linalotazamiwa kung’arisha Zanzibar mwezi ujao. “Ni wakati mgumu sana tunajua, lakini juu ya sababu zote! lengo letu ni kusonga mbele, pamoja na Sauti za Busara”, Yussuf Mahmoud anasema, Mkurugenzi wa Busara Promotions. “Tamasha hili ambalo kauli mbiu yake mwaka huu ni MOTO ZAIDI litaleta watu pamoja katika kusherehekea, kuwasaidia vijana wenye uwezo wa kiutamaduni, kuwapa bahati ya kukutana na wasanii wakubwa katika jukwaa moja na kutoa fursa ya kubadilishana mawazo kutoka kwa mmoja kwenda kwa mwingine. Lakini si hivyo tu, Inaweza pia kuwa fursa ya kubadilishana uzoefu, kufahamiana na pia Tamasha la Sauti za Busara linatuwezesha kuboresha utalii mpya wa kiutamaduni nchini Tanzania.”
Kama kawaida, tamasha hili hutokea kipindi cha sikukuu ya wapendanao hivyo kuongeza ladha zaidi. Kutoka viwanja vya watoto Kariakoo saa kumi kamili za jioni siku ya alhamisi tarehe kumi na moja februari kutakuwepo na maandamano makubwa na ya kipekee yatakayo ashiria ufunguzi rasmi wa tamasha hili la aina yake, wakiwemo wana sarakasi, mdundiko, ngoma na bendi, wote wakielekea Ngome Kongwe hadi itakapofika mida ya saa kumi na moja jioni. Kutoka hapo na kuendelea, kutakuwa na shoo za muziki kwa siku nne , pamoja na vikundi 40 (wanamuziki 400) akiwemo Thandiswa(Afrika Kusini), Nyota ndogo na Makadem (Kenya), Ba Cissoko (Guinea), Malick Pathe Sow (Senegal), Massar Egbari (Egypt), Banana Zorro, Fresh Jumbe, Chidi Benz (Tanzania) na wengi wengineo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269