Breaking News

Your Ad Spot

Feb 27, 2010

HITMA YA MAREHEMU MZEE KAWAWA YASOMWA KITAIFA LEO

RAIS Jakaya Kikwete akishiriki Hitma ya kitaifa ya Mmoja wa waasisi wa Taifa, marehemu Rashid Kawawa, iliyosomwa nyumbani kwa marehemu, Madale Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Sheikh wa mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa akisoma dua na kulia ni Vita Kawawa, mtoto wa marehemu. Kina mama wakiwa kwenye hitma hiyoWatoto wasliohudhuria wakipata chakula kwenye hitma hiyo.

Story
RAIS Jakaya Kikwete leo ameongoza viongozi, ndugu jamaa na Marafiki katika hitma ya 40 ya Mzee Rashidi Kawawa, nyumbani kwa marehemu, Madake nje ya jiji la Dar es salaam.
Kisomo cha hitma hiyo kiliongozwa na sheikh wa mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo naibu Waziri wa Nishati na Madini Adamu Malima na mtoto wa Marehemu, Vita Kawawa.
Kwa mujibu wa Vita, leo ndiyo siku ambayo simba wa Vita, alizawaliwa yaani  tarehe Februari 27, mwaka 1926. na pia imekuwa siku maalum zaidi kwa kuwa leo pia ni siku aliyozaliwa Mtume Muhammad (SAW) ambapo shamrashamra zilitawala Duniani kote kwa kusomwea Maulid usiku wa kuamkia leo.
Mzee Kawawa alifariki Dunia Desemba 31, mwaka 2009 mjini Dar es Salaa. Hitma yake ilikuwa awali isomwe Februari 16, mwaka huu, ikaahirishwa kwa kufuatia kifo cha Binti wa Mzee Kawawa  

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages