RAIS Jakaya Kikwete akiwa na Makamu wa Rais Dk. Ali Mohammed Shein na viongozi wengine waandamizi katika maziko ya Balozi Mwakawago kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo jioni.
Mwili wa marehemu, Balozi Mwakawago ukizikwa katika kaburi wakati wa mazishi hayo.
RAIS mstaa Benjamini Mkapa akifuatia
Rais wa awamu ya pili, Ali Hassani Mwinyi naye akimwaga udongo kumzika Mwakawago.
Stori
RAIS jakaya Kikwete leo amewaongoza mamia ya wananchi kumzika aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Daudi Nwakawago ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 71.
Balozi Mwakawago aliyefariki juzi, amezikwa leo jioni kwenye makaburi ya Kisutu Dar es Salaam, ambako Mbali na wananchi wa kawaida viongozi mbalimbali wakiwemo Marais wastaafu, Ali Hassani Mwinyi na Benjamin William Mkapa walikuwepo.
Kadhalika Mawaziri Wakuu Joseph Warioba na Dk Salim Ahmed Salim.
Marehemu, Mwakawago ameacha mjane na watoto watatu huku akiwa amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi kwenye baraza la mawaziri katika serikali ya awamu ya kwanza na ya pili na kuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269