STORY
Mamlaka ya hali ya hewa nchini imezishauri taasisi mbalimbali kuwa makini na athari zinazoweza kuletwa na mvua zinazoendelea katika maeneo mbalimbali nchini.Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Agnes Kijazi amesemahayo leo alipokuwa akizungumza na waandishio wa nahabari kuhusu mwelekeo wa hali ya mvua za masika katika kipindi cha mwezi Machi na Mei 2010.
Alisema kutokana na mvua zinazoendelea katika maeneo mbalimbali nchini kuna uwezekano mkubwa wa kuongezeka kwa vina vya maji kweye mabwawa na mito.
Hata hivyo Kijazi alisema rasilimali iliyokuwepo katika maeneo yenye uhaba wa mvua yatumike kwa uangalifu mkubwa.
Pia alizishauri kamati za maafa kuchukua hatua muafaka zitakazokabiliana na athari zitokanazo na na mafuriko,mmomonyoko wa ardhi na uharibifu wa miundombinu katika sehemu zinazotarajiwa kupata mvua za juu ya wastani.
Akizungumzia Sekta ya Afya Kijazi alisema kuna uwezekano mkubwa wa milipuko ya magonjwa ya kipindupindu na malaria kwenye maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani hususani maeneo ya kanda ya Ziwa na mikoa ya magharibi mwa nchi.
Alitoa angalizo kwa jamii kuwa mwaka huu ni mwaka wa El Nino na kusema kuwa haitarajii kuambatana na mvua kubwa kama za mwaka 1997/98 kwa sababu viashiria havionyeshi mwelekeo wa ongezeko la joto la maji ya bahari magharibi mwa bahari ya Hindi.
Pia kupungua kwa joto la maji ya bahari katika maeneo ya Indonesia huchangia kuleta mfumo wa ongezeko kubwa la mvua katika miaka ya El Nino.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269