Breaking News

Your Ad Spot

Aug 11, 2010

BASATA YAFANYA UCHAGUZI


Msimamizi wa Uchaguzi wa Shirikisho la Wanamuziki Tanzania,Yustus Mkinga (katikati) ambaye pia Ni Afisa Mtendaji Mkuu wa COSOTA,akitazama ubao wenye majina ya wagombea wa nafasi ya Rais wa Shirikisho la Wanamuziki Tanzania.Kulia kwake ni Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego na Rashid Masimbi,Mjumbe wa Bodi BASATA (kushoto).

stori

Hatimaye Shirikisho la Wanamuziki Tanzania leo (Jumatano) limepata viongozi wake wa muda katika uchaguzi uliofanyika kwenye Ukumbi wa BASATA na kusimamiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa COSOTA,Bw.Yunus Mkinga.

Katika uchaguzi huo uliokuwa wa vuta ni kuvuta,Bw.Ibra Washokera aliweza kuibuka kidedea kwenye nafasi ya urais baada ya kupata kura 12 na kumbwaga Mkongwe wa muziki wa dansi,Hamza Kalala ‘Komandoo’ aliyeambulia kura 2 tu.

Kwa upande wa nafasi ya Makamu wa Rais,Mwanamuziki wa muziki wa asili,Che Mundugwao aliibuka kidedea kwa kupata kura 9 na kuwaacha mbali wapinzani wake ambao ni Mkongwe Kassim Mapili na Gwalugano Ayoub walioambulia kura 3 kila mmoja.

Nafasi ya Katibu ilichukuliwa na Salum Mwinyi huku nafasi ya Mkurugenzi wa Fedha na Mipango ikikamatiwa na Samwel Semkuto.Aidha, wajumbe waliochaguliwa ni Samatha Rajab, Said Mukandara na George Mbata.


Wakiongea kwa kwa nyakati tofauti baada ya uchaguzi, Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego,Bw.Yustus Mkinga na Mlezi wa Mashirikisho ya wasanii,Mzee Rashid Masimbi walisema kwamba, kazi iliyopo mbele ni kwa viongozi hao kupanga mikakati ya muda mfupi na muda mrefu ya kuwaendeleza wasanii na kupigania maslahi yao.

Aidha, walisisitiza kwamba, kwa sasa wasanii wa muziki wanatakiwa kusimama imara chini ya shirikisho lao na kuwa na msimamo thabiti katika masuala mbalimbali yanayowahusu.

Kesho itakuwa ni zamu ya uchaguzi wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi na keshokutwa ni shirikisho la Sanaa Jongevu (Filamu),Wadau wote mnakaribishwa kwenye chaguzi hizo ambazo ni maendeleo makubwa kwa wasanii na sekta ya sanaa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages