WAFANYAKAZI wafagia barabara za Morogoro, Kawawa na Mlanzidi katika Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, wakiwa kwenye Ofisi za Manispaa hiyo leo, baada ya kugoma kufanya kazi wakishinikiza kulipwa mshahara wao wa amwezi uliopita. Wafanyakazi hao wapo chini ya mkandarasi wa usafi katika manispaa hiyo, kampuni ya Sweetconner.
MMOJA kati ya kina mama hao akilalamika
KINAMAMA ambao hufagia barabara za Mororogo, Kawawa na Mlandizi, Manispaa ya Kindoni, Dar es Salaam,leo wamechachamaa na kuamua kuandamana hadi kwenye ofisi za manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, kudai malipo ya mshahara wa mwezi uliopita.Wafanyakazi hao wanashinikiza ili mwajiri wao, kampuni ya Sweet Conner iliyochukua ukandarasi wa kufanya kazi hiyo katika manispaa ya Kinondoni, ilwalipe mshahara huo.
Mkururugenzi wa Kampuni hiyo, Christopher Mgonja, alikiri kutowalipa mshara hadi sasa,. akidai na yeye hajalipwa na Manispaa hiyo kwa miezi mitano sasa kisi cha sh. Milioni 30, kwa kuwa Manispaa hiyo inapaswa kumlipa sh. Milioni 60 kila mwezi.
Manispaa ya Kinondoni nayo ikakiri chelewesha malipo kwa mkandarasi huyo, kwa madai kwamba si kutokana na kuwa katika mchakato mbadala ambao ni mpya utakaowezesha wakandarasi kulipwa kulingana na kazi ilivyofanywa.
Ofisa uhusiano wa Manispaa hiyo, Sebastian Muhozya, alisema, malipo kwa mkanadarasi huyo yamekwama kufanyika baada ya kubaini kwamba Manispaa imekuwa ikipoteza fedha nyingi kuwalipa makandarasi wa ausafi viwango vya fedha ambavyo ni vikubwa kuliko kazi wanazofanya.
Alisema, zaidi ya sh, milioni 300 hupotea kila amwezi kutokana na malipo ya kazi za usafi ambazo hazikufanyika.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269