Breaking News

Your Ad Spot

Dec 15, 2010

CCM – UK YAFUNGUA SHINA JIPYA LUTON UINGEREZA

Mwenyekiti wa Tawi la CCM – UK,  Ndugu Maina  Owino, akitoa hotuba wakati  wa uzinduzi wa shina hilo.
Viongozi, ( waliokaa katikati) M/kiti Tawi UK aina Owino, kushoto mwenye kofia Katibu wa shina jipya Luton, Abraham Sangiwa na kulia ni M/kiti shina jipya Luton Albert Ntemi. Wliosimama toka kulia mwenye kofia Mjumbe shina jipya Sammy Martin, John Mwete, Kelvin Mjumbe wa London pamoja na Dr. Mmuhiza pia wa London  

Watanzania wengi walifurika Jiji la Luton Uingereza na kujiunga na chama cha mapinduzi katika ufunguzi wa shina jipya la Luton uliofanyika siku ya Jumapili Tarehe 12. 12. 2010 katika hoteli maarufu Chiltern UK.

Wengi wao wasema wana imani kubwa na CCM katika kuiongoza Tanzania kwa kuonyesha mwelekeo wa kuwa na imani na Vijana wasomi wachapakazi walioko ndani na nje ya nchi.

Ufunguzi huo ambao uliongozwa na Mwenyekiti wa Tawi la CCM – UK Ndugu MAINA OWINO kwa kushirikiana na viongozi wengine wa chama akiwemo Katibu Uenezi wa siasa Bwana Moses Katega. Pia Viongozi kutoka mashina ya Reading, Birmingham na Sehemu zote za London walijumuika pamoja.

Katika hotuba yake fupi Ndugu MAINA OWINO alitoa changamoto nyingi za mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano iliyopita chini ya Uongozi wa Mwenyekiti CCM Taifa na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa JAKAYA MRISHO KIKWETE katika nyanja mbalimbali kama Madini,Elimu, ukusanyaji wa mapato ya serikali, waajiriwa wenye sifa za kukidhi nafasi za uongozi serikalini katika nyanja zote na ujasialiamali kwa watanzania wanaojitafutia maendeleo bila bugudha.

Changamoto kuhusu ushiriki wa vijana wasomi hapa UK kuingia katika mchakato wa siasa ndani ya chama ili kuleta mabadiliko yatakayozidi kukiimarisha chama kisera, mwelekeo na kuzidi kuwaletea watanzania maendeleo katika nyanja mbalimbali kupambana na kupambana na umasikini yalitolewa na Katibu wa shina jipya la Luton aliyechaguliwa siku Ndugu ABRAHAM SANGIWA na kuungwa mkono na wajumbe wote waliohudhuria ufunguzi huo

Viongozi Waliochaguliwa siku hiyo ni:

ALBERT NTMI – MWENYEKITI

ABRAHAM SANGIWA – KATIBU MKUU

JOHN MBWETE – MJUMBE

SAMMY MARTIN – MJUMBE

NORMAN WAGE - MJUMBE

1 comment:

  1. Mambo ya vyama mpaka huko nje, mimi nilidhani mkiwa huko hakuna cha vyama, wote ni tanzania! Ok, sio mbaya

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages