Breaking News

Your Ad Spot

Dec 22, 2010

NUNDU AWASHUKIA WATUMISHI TPA WANAOTAKA UTAJIRI WA HARAHARAKA KWA NJIA YA RUSHWA

WAZIRI wa Uchukuzi Omari Rashid Nundu (kushoto) na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mhandisi, Athumani Mfutakamba (wapili kushoto), wakimsikiliza kwa makini Meneja  wa Kitengo cha Kuhudumia makontena bandarini (TICTS), Donald Talawa (kulia) akiwaeleza kitengo hicho kinavyofanya kazi zake, alipotembelea kituo cha kitengo hicho, kilichopo Ubungo, Dar es Salaam, jana.
WAZIRI wa Uchukuzi Omari Rashid Nundu (kushoto) akikagua kituo cha kuhuhudumia makontena bandarini cha kampuni ya AMI, alipofanya ziara ya kukagua shughuli zinazohusiana na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) mjini Dar es Salaam, jana. Wapili ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Grant Lendrum. 
Mawakala wa kutoa magari bandarini wakitoa dukuduku lao mbele ya waziri Nundu katikaziara hiyo.
====================================

HABARI KAMILI

WAZIRI wa Uchukuzi, Omari Rashid Nundu ametaka mfanyakazi yeyote mwenye lengo la kujipatia utajiri wa haraka ikiwemo kwa njia ya rushwa katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ajitoe haraka katika mamlaka hiyo.


Pia ametaka kufanya hivyo mfanayakazi wa malaka hiyo atakayeona hawezi kwenda na kasi ya sasa ya utendaji kai wenye ufanisi wa hali ya juu anayotaka ambayo ametaka utekelewaji wake uwe umefikiwa katika kipindi cha mizi sita kuania sasa.

Akiunguma jana mjini Dar es Salaam, wakati wa majumuisho ya iuara yake ya sikuy mbili, kukagua shughuli mbalimbali za kazi na utekelezaji wa majukumu ya mamlaka hiyo, Waziri Nundu alisema kuania sasa ni lazima utendaji wa wafanyakai wa TPA uingatie maadili ya utumishi wa umma na matakwa ya wateja.

"Hii ina maana kwamba mawasiliano na wateja yawe ya haraka sana na yenye tija ya hali ya juu. Utendaji uwe wenye kuzingatia matakwa makuu ya mteja, nayo ni ufanisi wa hali ya juu ndanii ya ajenda moja tu kutoa huduma ya kuendeleza nchi bila masharti ya wazi au yaliyofichika. Vishawishi ni vingi hasa katika kutunuku miradi, hivyo tusishawishike kwa rushwa kutafuta utajiri wa haraka haraka", alisema Wairi Nundu.

Watumishi wa Mamlaka ya Bandari Tanania, wamekuwa wakishutumiwa baadhi yao kujihusisha na rushwa, wizi au upotefu wa vifaa kwenye magari, katika utendaji wao wa kazi, jambo ambalo limedaiwa kuvunja ari kwa baadhi ya nchi kutopitisha sasa mizigo katika badari hapa nchini.

Waziri Nundu ambaye aliambatana ba Naibu Waziri wake, Mhandisi Athumani Mfutakamba, aliwataka wafanyakazi wa TPA, kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM na maelekezo ya viongozi kwa nguvu zao zotena kuchangia kwa dhati kuifanya Tanzania kuwa lango la biashara kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.

Aliagiza kuanza mara moja kujenga na kuimarisha miundombinu ya bandari kwa kuzingatia mpango mkuu wa TPA, ambao ni dira ya kutekeleza na hatimaye kufukiwa lengo hilo la kuifungua nchi kuwa lango kuu la biashara kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati lengo ambalo alisema bila Tanzania kuwa na bandari zenye ufanisi mkubwa haiwezi kulifikia.

Waziri Nundu aliagiza utekelezaji huo, uanze mara moja kwa matayarisho thabiti na upambe kasi barabara kuanzia mwaka wa fedha wa 2011/2012 na kuwataka wafanyakazi wa TPA kufanya juhudi za makusudi kuhakikisha wate waliozihama bandari za Tanzania wanarudi tena kuzitumia,

"Hii ina maana kwamba jitihada za makusudi kwa kushirikiana na wadau wengine kama TAZARA na TRL zifanywe kwa lengo la kuongeza ufanisi wa mtandao wa uchukuzi nchini na hivyo kuwarudisha wateja hawa ambao ni kutoka Uganda na Zambia" alifafanua waziri Nundu.


Aliagiza kwamba, wakati mkakati wa ujenzi wa bandari ya Mwambani, Tanga, ukiendelea kupangwa, Bandari ya Tanga ipatiwe vifaa ambavyo vitaongeza ufanisi wa matumizi ya bandari hiyo na kwamba vifaa hivyo vinajulikana na havina gharama kubwa na kutaka agizo hilo litekelezwe kabla ya Julai 2011.

Waziri aliitaka TPA kuanza mawasiliano na uongozi wa mkoa wa Tanga, ili maeneo ndani na nje ya bandari ambayo yanatumika kwa shughuli zisizo za kibandari zichukukliwe na kumilikishwa Mamlaka hiyo na maeneo ya bandari yaliyokwishachukuliwa yapatiwe hati miliki kuondoa uwezekano wa kuvamiwa na wananchi, na kuwa maeneo hayo ni yapo Mwambani Tanga na Mtwara.


Aliagiza pia upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa eneo la Kisarawe kwa ajili ya matumizi ya kuhifadhi mzigo ufanyike mara moja hata kama ni kwa gharama za serikali na kama haitawezekana kabla ya mwaka wa fedha wa 2010/2011 eneo taratibu zifanywe ili limilkikiwe na serikali kuoitia TPA.


Katika ziara hiyo, jana Waziri Nundu alikagua vituo vya bandari za nchi kavu vya kuhifadhi makontena na vya magari kutoka bandarini, vilivyopo Kurasini, Chang'mbe na kimoja kipya kilichopo eneo la Gerezani, ambacho kitaanza kazi Januari mwakani.

Kwenye vituo hivyo, Upandishwani wa gharama za kutoa magari kwa mbinu mbalimbali ikiwemo maofisa kuchelewesha kwa makusudi kutoa vibali kwa muda unaotakiwa na badala yake kutoa vibali hivyo baada ya siku zinazowalazimu wahusika kulipia pia gharama za utunzaji magari.

Wateja ambao waziri aliwakuta kituo cha Farion Trading Limited, walimwambia Waziri kwamba baadhi ya maofisa kwenye kampuni hiyo wamekuwa wakifanya ucheleweshaji wa makusudi kutoa vibali, jambo ambalo huwalazimu kulipia gharama zaidi.

1 comment:

  1. Rushua au rushwa ni sumu isiyoogopewa nchini, viongozi wanakemea, lakini wapi, kwasababu `utamu wake' kwa mlaji ..mmmh, ni kama asali, lakini madhara yake mmmh, ni kama sumu inayoua taratibu,..........

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages