Rais Kikwete akimvisha nishani Mama Maria Nyerere |
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana Phillemon Luhanjo imesema, tunuku hizo zilikuwa sehemu ya sherehe za Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara ambazo zilifikia kilele chake Desemba 9, 2011, na zimetolewa katika sherehe iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
Nishani alizotunuku Mheshimiwa Rais Kikwete ziko katika makundi matatu ambayo ni Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo hutolewa kwa Marais Wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao waliingia madarakani kwa njia za kikatiba na wameendelea kuonyesha maadili mema yenye nidhamu, heshima na mfano wa kuigwa.
Nishati ya pili ni Nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Pili inayotolewa kwa Makamu wa Rais na Mawaziri Wakuu Wastaafu walio hai ama marehemu na walioondoka madarakani bila kashfa na hata baada ya kuondoka katika madaraka wameendelea kuwa na maadili mema na kuishi kwa heshima na maadili ya Ofisi yao.
Nishati ya tatu iliyotolewa ni Nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Nne ambayo hutolewa kwa raia ambao walishiriki katika harakati za kupata uhuru na walionyesha vitendo thabiti vya kizalendo katika kipindi cha miaka 50 ya Uhuru na wameendelea kuonyesha maadili mema ya kusifika na kuigwa. Nishani hiyo pia hutolewa kwa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais Mstaafu wa Awa,u ya Pili Ali Hassani Mwinyi akivishwa nishani na Rais Kikwete
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa akivishwa nishani na Rais Kikwete
Waziri Mkuu mstaafu, Salim Ahmed Salim akivishwa nishani na Rais. Picha kutoka BLOGU YA KAMANDA WA MATUKIO
Rais Mstaafu wa Awa,u ya Pili Ali Hassani Mwinyi akivishwa nishani na Rais Kikwete
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa akivishwa nishani na Rais Kikwete
Waziri Mkuu mstaafu, Salim Ahmed Salim akivishwa nishani na Rais. Picha kutoka BLOGU YA KAMANDA WA MATUKIO
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269