Breaking News

Your Ad Spot

Dec 9, 2011

MTAALAMU WA HALAIKI KATIKA SHEREHE ZA KITAIFA AFARIKI DUNIA


 Msanii maarufu Bw. Lawrence Hinju ambaye kwa miaka mingi amekuwa mahiri katika kuandaa halaiki kwa ajili ya sherehe mbalimbali za kitaifa amefariki dunia.

Taarifa iliyotolewa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) zimesema, Hinju amefariki usiku wa kuamkia Alhamisi ya 07/12/2011 nyumbani kwake Mwananyamala jijini Dar es Salaam, kutokana na kuugua kifua.

"Marehemu alianza kuugua Kifua wiki tatu zilizopita akiwa Uwanja wa Uhuru kwenye maandalizi ya Halaiki ya watoto kwa ajili ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara" ilisema taarifa hiyo.

Ilisema Mbali na ubobezi katika kuandaa halaiki hizo za matukio ya kitaifa, alikuwa Mwajiliwa wa Baraza la Sanaa la Taifa toka Tarehe 01/07/1988 hadi mauti yalipomfika.

Aidha, Marehemu Lawrence Hinju aliteuliwa kuwa mjumbe wa Bodi ya Baraza la Sanaa la Taifa kuanzia mwaka 2005 hadi sasa.

"Kwa niaba ya Baraza la Sanaa la Taifa, wasanii na wadau wa Sanaa hasa katika upande wa Sanaa za Ufundi, tunatoa pole kwa wote walioguswa na msiba huu", imesema Basata katika taarifa hiyo na kuongeza.

"Ni wazi pengo lililoachwa na Marehemu halitaweza kuzibika kamwe kwani amekuwa nguzo muhimu katika kufanikisha sherehe mbalimbali za kitaifa".

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mwili wa Marehemu unatarajiwa kusafirishwa Siku ya Jumamosi Tarehe 10/12/2011 kwenda kuzikwa nyumbani kwao Mkoani Ruvuma. Taratibu za usafiri zinafanyika nyumbani kwa dada yake Yombo Relini (Kwa Ali Mbowa).

Taarifa imetolewa na
Materego
KATIBU MTENDAJI
BASATA

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages