Na Rose Jackson,Arusha
WAANDISHI wa habari wametakiwa kutambua kuwa wana wajibu wa kufuatilia na kuifahamu vyema katiba na mapungufu yaliyomo ili waweze kuielimisha jamii umuhimu wa kushiriki katika mchakato wa kutoa maoni ya katiba hiyo
Sanjari na kuhakikisha kuwa wanazifahamu sera za nchi zinazotungwa ili waweze kufichua mapungufu yaliyomo ndani ya sera hizo.
Hayo yamesemwa na mkurugenzi mtendaji wa umoja wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania(UTPC) bw Abubakari Karsan alipokuwa akifungua mafunzo ya siku nne ya kwa wanachama waandishi wa habari wa Arusha press club( APC) yanayohusiana na ufuatiliaji wa sera na matumizi ya pesa za umma yaliyofanyika mjini hapa.
Alisema kuwa waandishi wa habari wanapaswa kuifahamu katiba na malengo yake muhimu kwa kuwa wako baadhi ya waandishi hawajui na kutambua umuhimu wake hali inayowapelekea kushindwa kuelimisha jamii juu ya mchakato mzima wa katiba.
“nawaombeni sana waandishi muwe mhimili katika kuielewa kwanza katiba na mkishaielewa nyie nyie muwe mfano mzuri wa kuigwa kwa kuhakikisha kuwa wananchi wanaielewa katiba vizuri kwa kutumia kalamu yenu”alisema Karsan
Sambamba na hilo Karsan aliwataka waandishi kuifahamu kikamilifu sera mbali mbali zinazotungwa ili waweze kuibua mapungufu ambayo hayatekelezwi na baadhi ya watu.
“sera ziko za aina mbali mbali kama za afya,elimu,maji na nyinginezo hivyo ili kuipa jamii taarifa sahihi ni vema waandishi wakazijua kwanza sera hizo ili ziwasaidie kufichua mapungufu ambayo hayatekelezeki katika sera hizo”aliongeza
Aidha aliwataka waandishi hao watakapopata mafunzo hayo hawana budi kufichua maovu ya matumizi mabaya ya fedha za umma katika Halmashauri nyingi nchini huku akitolea mfano Halmashauri ya Kishapu ambayo imekuwa na hati mbaya ya matumizi ya fedha za Serikali
Kwa upande wake mwezeshaji wa mafunzo hayo bw Pantaleon Shoki alisema mafunzo hayo yatawasaidia waandishi kuifahamu sera ambapo wao wataweza wakawaelimisha wananchi umuhimu wa sera na kwa namna inavyotumika ambapo pia wataweza kubaini sera ambazo hazitekelezeki kwa jamii.
Alisema kuwa waandishi wa habari wana nafasi ya Kuanzisha midahalo maalum ya kisera kwa ajili kujadili sera mbalimbali ili wananchi na wadau waweze kufahamu sera hizo na kama zina mapungufu waweze kupaza sauti kwa serikali ili iweze kutekeleza sera hizo.
Aidha bw Shoki aliwasihi wanahabari hao kutumia mafunzo hayo vizuri katika kuhakikisha kuwa wanafuatilia bajeti zinazopangwa na kubaini makosa yake ili waweze kuifikishia jamii taarifa zilizo sahihi.
Your Ad Spot
Jun 10, 2012
Home
Unlabelled
WAANDISHI WA HABARI WAFUNDWA KUIFAHAMU KATIBA
WAANDISHI WA HABARI WAFUNDWA KUIFAHAMU KATIBA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269